Msanii wa muda mrefu kutoka Marekani Rick Ross amewaacha mashabiki wake kutoka ukanda wa Afrika Mashariki wakiwa na kiu kikuu kwa kudokeza kwamba huenda akashirikishwa kwenye remix ya ngoma ya Navy Kenzo kutoka Tanzania, Sip N Whine.
Ross alikuwa na mazungumzo ya moja kwa moja kupitia mtandao wa Instagram na kundi hilo la Navy Kenzo ambapo alikuwa akiwapa maua yao kuhusu ukali wa wimbo wa Sip N Whine ambao ni miongoni mwa nyimbo nzuri tu zilizopo kwenye albamu yao ya Most People Want This.
Iwapo hili litafanikiwa, hii itakuwa collabo ya pili kwa msanii huyo wa kimataifa kufanya na wasanii kutoka Tanzania.
Ifahamike kwamba Diamond Platnumz mwaka 2018 alifanikiwa kuweka rekodi kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kufanya collabo na Ross.
Ross ambaye ni mmiliki wa Bel Air, shirika la ndege ambalo pia wasanii wa Navy Kenzo ni mabalozi wake aliisifia ngoma hiyo akisema kuwa ni nzuri na angependa kushirikishwa kwenye remix yake.
“Napenda ngoma yenu, ina vibe moto na ningependa kuwaeleza kwamab kuna nafasi ya Rick Ross kushiriki ili tuifanyie remix. Niko na furaha kufanya hivyo na nyinyi,” Ross aliwaambia Aika na Nahreel ambao ndio wanaounda kundi la Navy Kenzo.
Rick Ross aliukubali sana wimbo wa Sip N Whine ambamo humo ndani wasanii hao wametaja Bel Air, kampuni ya ndege ambayo Ross ni mmoja wa wamiliki wake.