logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Baraka zazidi kutiririka kwa mwalimu aliyemshonea mwanafunzi sare darasani Narok

Mcheza densi Edward Mbaria anayefahamika kwa jina Lit Boy amtuza mwalimu Joyce Malit.

image
na

Makala12 May 2023 - 08:11

Muhtasari


• Mcheza densi huyo alimtembelea mwalimu huyo aliyenoekana katika picha zilizoenea kwenye mtandao wa kijamii akimshonea nguo mwanafunzi wake.

Mcheza densi wa kushtukiza Edward Mbaria anayefahamika kwa jina Lit Boy amemtuza mwalimu Joyce Malit ambaye picha yake ilinenea akimshonea mwanafunzi wake sare darasani.

Lit Boy ambaye ana ufuasi mkubwa kwenye mtandao wa TikTok, Alhamisi aliizuru kaunti ya Narok kwa ajili ya kumzawadi mwalimu huyo ambaye alionekana kumshonea mwanafunzi wa kike sare yake iliyokua imechanika.

Katika picha hiyo ambayo imemzolea mwalimu huyo sifa kochokocho, alionekana darasani amemvisha leso huku akimshonea mwanafunzi wake sare ambayo ilikuwa imeraruka.

Lit Boy aliyetangaza taarifa hio kwenye akaunti yake ya Instagram alisema kuwa alishirikiana na benki ya I&M katika kumzawadi mwalimu huyo.

“Mimi na benki I&M Tulishirikiana Kumtuza Mwalimu Wetu Mpendwa Madam Joyce Sempela Malik na hisia zake zilikuwa za Thamani 😭” Lit Boy aliandika.

Picha ya msichana huyo na mwalimu wake imevutia watu kwenye mitandao ya kijamii, huku wengi wakionyesha kufurahishwa na kujitolea kwa mwalimu huyo na nia ya Sonko kuingilia kati na kutoa usaidizi.

Mwalimu huyo ameweza kuzawadiwa na atu kathaa maarufu akiwemo aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved