logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mchungaji Size-8 afichua sababu ya kuogelea kwenye bwawa akiwa na nguo ndefu

"imi niko tayari unajua mimi ni mchungaji na kwa hiyo siwezi enda kubadilisha mavazi"

image
na Radio Jambo

Habari16 May 2023 - 09:23

Muhtasari


• “Hizi ni stori gani manze, hii ni nini sasa hata kama ni kuwa pasta, lazima tusapoti wake zetu lakini mambo mengine hapana,” DJ Mo alilalama.

Mchungaji Size 8 afichua sababu ya kuogelea na nguo ndefu

Msanii ambaye pia ni mchungaji Size 8 amefichua sababu ya kutovalia mawanda ya kuogelea walipokuwa katika mtoko na mume wake DJ Mo kwenye bwawa.

Size 8 alipakia video kwenye ukurasa wake wa Instagram alipakia video wakiwa na mume wake kando ya bwawa.

DJ Mo alimsihi mkewe ajiunge naye kwenye kuogelea kama njia moja ya kujivinjari kama wanandoa lakini alipigwa na butwaa mkwe alipokubali kujiunga naye kweye bwawa lakini akasema hawezi vua vazi alilokuwa amelivaa ili kuvalia vazi la kuogelea.

Size 8 alitoa kisignizio kwamba hawezi kuvaa vazi la kuogelea ambalo linaonesha sehemu kubwa ya mwili wa mtu hadharani, kwani yeye ni mchungaji na anafaa kujisitiri vyema katika mazingira yoyote.

“Kuwa mtumishi wa Mungu ni gharama....... Ama mnaona aje?....Mimi nitaogelea hivi nilivyo mpenzi wangu, niko sawa. Mimi niko tayari unajua mimi ni mchungaji na kwa hiyo siwezi enda kubadilisha mavazi na kuvaa vazi la kuogelea. Unajua hatufai kuonesha miili yetu sana kwa hiyo lazima tuingie hivi kama tunaogelea,” Size 8 alisema.

DJ Mo alionesha kutofurahishwa na kitendo cha mkewe Size 8 na kuuliza ni nini hicho kwani yeye alitarajia kujivinjari na mkewe wakiwa katika mavazi ya kuogelea.

“Hizi ni stori gani manze, hii ni nini sasa hata kama ni kuwa pasta, lazima tusapoti wake zetu lakini mambo mengine hapana,” DJ Mo alilalama.

Video hiyo iliisha pale ambapo Mo alimlazimisha mkewe kuondoka majini ili kwenda kuvalia mavazi ya kuogelea.

Hii hapa video yenyewe:

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved