logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kwa nini 'Stella' ni gumzo kubwa sana nchini Kenya kila mwaka Mei 17?

Mwamburi katika mahojiano ya awali alikiri kwamba ni hadithi ya kweli na si ya kubuni.

image
na Radio Jambo

Makala17 May 2023 - 04:33

Muhtasari


• Mwamburi katika wimbo wake wa ‘Stella Wangu’ ambao aliutunga Zaidi ya miaka 30 iliyopita, alihadithia kwa majonzi jinsi Stella alivyomtenda.

Freshley Mwamburi na 'Stella' wake.

Tarehe 17 Mei aghalabu huwa mada inayovuma kila wakati nchini Kenya haswa kwenye mitandao ya kijamii.

Mei 17 ni tarehe ya kipekee kwa wengi wa Wakenya mitandaoni kwa sababu siku zote itakuwa siku ambayo huzuni ya kwanza ya Mkenya kuwahi kurekodiwa ilikuja kuwa.

Siku hii huwa gumzo haswa kwa kurejelea maisha ya msanii mkongwe Freshley Mwamburi ambaye mapema miaka ya 90s alirekodi wimbo baada ya mrembo wake kumpiga changa la macho.

Mwamburi katika wimbo wake wa ‘Stella Wangu’ ambao aliutunga Zaidi ya miaka 30 iliyopita, alihadithia kwa majonzi na huzuni mwingi jinsi alivyojitoa kwa hali na mali; udi na uvumba ili kuhakikisha mpenzi wake – Stella amesafiri kwenda Japan kusomea udaktari.

Mwamburi katika wimbo huo ambao aliufanyia remix kwa mtindo wa Reggae miaka michache iliyopita alikiri kuuza mali yake yote kufadhili masomo na nauli ya ndege kwa Stella lakini baada ya miaka miwili mrembo alirudi Kenya akiwa na mtoto mkononi na nyuma yake akifuatwa kwa ukaribu na mwanamume raia wa Japan ambaye Mwamburi alimtaja kuwa mbilikimo mwenye urefu wa futi nne.

Aliendelea kumpenda Stella, lakini kwa sababu mambo mazuri hayadumu, uhusiano wao ulijaribiwa haraka haraka baada ya msichana huyo kumgonga kwa taarifa kwamba alikuwa akisafiri kwenda Japan kuongeza masomo yake.

Katika mahojiano ya awali na runinga ya KTN, Mwamburi alisema ilikuwa hadithi ya kweli na ni tukio ambalo lilimkwapua moyo pakubwa kiasi kwamba aliamua kumaliza huzuni wake katika kutunga wimbo huo.

Mwaka huu, Mei 17 ambayo ni Jumatano inaadhimisha miaka 31 tangu huzuni hiyo, na huku Mwamburi akiendelea kuponywa kutokana na huzuni hiyo, Wakenya kwenye Twitter - katika hali yao ya kawaida - wana maneno machache ya kusema, baadhi wakizua utani wa aina yake kumhusu Stella.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved