logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mcheshi Erick Omondi aponea kifo baada ya kuhusika kwenye ajali katika eneo la Suswa

Eric Omondi aponea kifo baada ya gari alimokua akisafiria kuharibika.

image
na Radio Jambo

Makala16 May 2023 - 05:14

Muhtasari


• Vincent Mboya katika akaunti yake ya Instagram alichapisha video ya gari lililokokotwa, huku Eric Omondi akiwa bado ndani ya gari hilo.

• "Leo karibu tupoteze maisha. Tunamshukuru Mungu tulikuwa hatusafiri kwa kasi ya juu." Ilisoma sehemu ya ujumbe huo wa Vincent.

Vincent Mboya na mcheshi Erick Omondi

Mcheshi Eric Omondi ambaye sasa amegeuka na kuwa mwanarakati aponea kifo baada ya gari alimokua akisafiria kuharibika.

Mcheshi huyo maarufu wa Kenya Eric Omondi na rafiki yake Vincent Mboya walijipata katika hali ya kutisha baada ya gari la Mercedes Benz walimokuwa wakisafiria lilipoharibika usiku wa kuamkia leo karibu na Suswa Narok.

Vincent Mboya katika akaunti yake ya Instagram alichapisha video ya gari lililokokotwa, huku Eric Omondi akiwa bado ndani ya gari hilo, video hio iliambatana na maombi ya kushukuru kwa kunusurika.

"Leo karibu tupoteze maisha. Tunamshukuru Mungu tulikuwa hatusafiri kwa kasi ya juu." Ilisoma sehemu ya ujumbe huo.

Ajali hiyo inajiri saa chache baada ya Eric Omondi kusitisha shughulu katika Barabara ya Langata, na kuwahamasisha watu kuhusu gharama ya juu ya maisha nchini Kenya.

Wakati wa maandamano hayo, aliwagawia watu unga wa ugali, huku akiangazia changamoto zinazowakabili raia wa kawaida huku hali ya uchumi ikiendelea kuwa mbaya.

Mabadiliko ya Eric Omondi kutoka kuwa mcheshi hadi kuwa mwanaharakati wa haki za kiraia yamenasa hisia za umma. Kwa miaka mingi, amethibitisha kuwa zaidi ya mtumbuizaji tu, akitumia jukwaa lake kuangazia masuala ya kijamii yanayowahusu Wakenya.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved