logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mimi silipishi ili kutoa msaada kwa mtu yeyote - Sonko asema baada ya kuonesha pesa nyingi

“Usitume pesa kwa pikipiki, hakuna pikipiki mimi napatiana." - Sonko.

image
na Davis Ojiambo

Burudani17 May 2023 - 13:16

Muhtasari


  • • "Siitishi mtu pesa ya kujisajili au ya kitu chochote, msaada kutoka kwa Sonko ni bure bila ada yoyote kwa umma,” Sonko alisema.
Sonko awaonya wafuasi wake kuhusu matapeli.

Mhisani na mwanasiasa Mike Sonko siku moja baada ya video yake akijigamba na pesa nyingi kuenezwa, amesema kuwa yeye huwa hatozi kiasi chochote cha ada ili kutoa msaada kwa mtu yeyote mweye uhitaji.

Sonko alipakia video kwenye kurasa zake mitandaoni akiwatahadharisha umma kwamba kuna watu wamejitokeza wakitumia jina lake na kudai kwamba wanatoa misaada ya kifedha kwa watu wenye uhitaji kumbe ni walaghai.

Sonko alisema kuwa atakuwa anatoa tahadhari hiyo kila siku ili kuwaokoa watu ambao wamekuwa wakilalamika kulaghaiwa pesa na watu wanaojihusisha na yeye.

 Mwanasiasa huyo mwenye mazoea ya kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji mbalimbali alisema kuwa msaada wake yeye hutoa bila kuitisha hongo yoyote.

“Usitume pesa kwa pikipiki, hakuna pikipiki mimi napatiana. Kama ni kusaidia huwa nasaida bure. Siitishi mtu pesa ya kujisajili au ya kitu chochote, msaada kutoka kwa Sonko ni bure bila ada yoyote kwa umma,” Sonko alisema.

Sonko alifichua kwamba walaghai hao wamefikia hatua nyingine ya kuwaajiri wasichana kujifanya ndio makatibu katika ofisi ya Sonko ili kuitisha pesa kutoka kwa watu wenye uhitaji kabla ya kupokea msaada, kumbe ndio mwanzo wanafyonza kile kidogo walichobaki nacho.

Sonko amejitokeza kuzungumzia maswala ya pesa siku moja baada ya kuonekana akijigamba na pesa zake nyingi ambapo ilikisiwa alikuwa anamjibu jamaa mmoja aliyemghasi.

Kwenye video hiyo, Sonko alisikika akijigamba kwamba shilingi milioni mbili taslimu za Kenya alizokuwa nazo ni kidogo kwake kwani ni kama hela za mfukoni tu kwa ajili ya matumizi madogo kama kuweka gari lake mafuta.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved