Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Bonfire Adventures Simon Kabu, ameahidi kumzawadi mtoto mwenye umri wa miaka mitatu ambaye alienea mitandaoni kutokana na uwezo wake wa kuyataja majina ya wanasiasa kwa usahihi.
Simon Kabu alisema kuwa anataka kumpeleka mvulana huyo mchanga kwa likizo ya siku tatu katika mji wa Mombasa.
Kijana huyo alionyesha uwezo wake wa kuwataja wanasiasa kadhaa wa Kenya wakiwemo maseneta na magavana bila kutokwa na jasho.
Baadhi ya viongozi aliowataja katika video hiyo ni rais wa Kenya, naibu rais, mwanasheria mkuu na mkuu wa mawaziri.
"Rais wa Kenya - William Ruto, Naibu wa Rais - Rigathi Gachagua, Mwanasheria mkuu- Justin Muturi, Gavana wa Murang'a - Kang'ata wa barua, Mbunge wa Kigumo -Joseph Munyoro, Gavana wa Kirinyaga - Anne Waiguru, Gavana wa Kiambu - Kimani Wamatangi, Mbunge wa Kapseret - Oscar Sudi, Gavana wa Mombasa - Abdulswamad Shariff," kijana huyo alisema.
Video hiyo ilisambaa mitandaoni na kuwaacha Wakenya wakiwa na mshangao.
Baadhi yao walikua na haya yakusema;
Cindyshe67: Mimi hata mbunge wetu wa Budalang'i simjui jina.
Joesiecand: Alipiwe fees na holiday pia ......ππππ
Mercy_cheruno1: najua president pekee πππwueh
Marion_nasimiyu_: mimi hata sijui chief wa kwetu ghaaasi I need my brains back
Je? Wewe wayafahamu majina ya viongozi wangapi?