logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KRG- Octopizzo alinunua views za Youtube

KRG the Don amemkashifu rapa Octopizzo akidai kuwa mwanamziki huyo si maarufu Kenya.

image
na

Yanayojiri26 May 2023 - 06:47

Muhtasari


• Akizungumza kwenye video ya moja kwa moja katika akaunti yake ya Instagram KRG alisema kuwa umaaarufu wa Octopizzo nchini Kenya umeisha.

• KRG aliongeza kuwa wasanii maarufu Kenya ni yeye na Dufla peke yake.

KRG the Don na Octopizzo

Msanii Karagu Kimani almaarufu KRG the Don amemkashifu rapa Octopizzo na kusema kuwa mwanamziki huyo si maarufu Kenya.

Akizungumza kwenye video ya moja kwa moja katika akaunti yake ya Instagram KRG alisema kuwa umaaarufu wa Octopizzo nchini Kenya umeisha.

“Octopizzo hakuna ata mtu anamjua akieza tembea mtaani, saizi labda awadanganye wazungu ambao hawamjui kuwa yeye ni msanii maarufu.” KRG alisema.

Dufla na KRG walidai kuwa Octopizzo alizinunua 'views' za Youtube wakiongeza kuwa wimbo wake Octopizzo ulikuwa na views nyingi lakini haukua ukitrend kwenye Youtube.

Alisema kuwa Octopizzo na wasanii wa Bongo Harmonize na Diamond wanahusika na kununua Views za Youtube.

" Octopizzo, Harmonize na Diamond wananunua 'Views', siezi kumbuka ata nyimbo moja ya Octopizzo mimi, ilikuwa muda wa 'Curfew' niliposkia wimbo wake wa mwisho akiwa msanii anayeibuka." 

Walimkashifu Octopizzo wakiwa na rafiki yake Dufla na kusema kuwa aliacha kutoa mziki licha ya msanii huyo kuachilia mziki wake mpya Alhamisi tarehe 25, Mei.

Aliongeza kuwa wasanii maarufu Kenya ni yeye na Dufla peke yake.

“Saizi ni wasanii wawili peke yake maarufu Kenya, mimi na Dufla,” aliongeza KRG.

Wimbo mpya wa Octopizzo ‘Sijawai’ umepata zaidi ya “views” za Youtube Zaidi ya milioni moja ndani ya siku moja pekee yake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved