logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mustafa aomba msaada tena ili kumalizana na tatizo la afya ya mama, "Nahitaji kama 1.5m"

“Tuko sehemu nzuri angalau lakini tuseme tukipata milioni moja au milioni moja na nusu hivi ..."

image
na Radio Jambo

Habari27 May 2023 - 08:44

Muhtasari


• Mustafa alisema kuwa pindi tu afya ya mama yake itaimarika kupitia michango ya watu, basi atarejea katika muziki.

• Msanii huyo pia alikiri kwamba hayupo katika mahusiano yoyote kwani alipoteza ujasiri wake wa kiume baada ya video yake kusambaa.

Msanii mkongwe kutoka Ogopa Djs, Coonel Mustafa

Msanii mkongwe kutoka humu nchini Colonel Mustafa ameibuka akidai kwamba angalau ameanza kuona mwanga mwisho wa handaki katika suala zima la afya ya mama yake.

Ikumbukwe wiki kadhaa zilizopita baada yake kuonekana akiwa anafanya kazi ngumu ya mikono, wengi walimhurumia na kujitokeza kwa wingi kumpa msaada wa kifedha, haswa aluipofichua kwamba alilazimika kufanya mjengo ili kumhudumia mama yake ambaye anaugua saratani.

Msanii huyo wa kitambo wa ‘Monalisa’ alipatiwa mchango wa Zaidi ya shilingi milioni moja lakini sasa ameibuka akisema kuwa japo mambo yamenaza kutengemaa upande wake lakini bado ana uhitaji Zaidi wa angalau milioni moja na nusu ili kumalizana na tatizo la afya ya mama yake kabisa.

Katika mahojiano na chaneli ya Goldmine, Colonel Mustafa aliwashukuru wengi waliojitokeza kwa wingi kumpa msaada wa kifedha na kuwasihi wasichoke kuendelea kusimama naye kwa ajili ya afya ya mama yake.

“Tuko sehemu nzuri angalau lakini tuseme tukipata milioni moja au milioni moja na nusu hivi tutamalizana na tatizo la mama yangu. Mama atapata kutibiwa kabisa na sasa hapo kama ni muziki nitajisimamia na kama ni kazi mtanipatia nitajishughulikia,” alisema.

Awali katika mahojiano na kituo kimoja cha redio, Mustafa alikiri kwamba alikuwa ameacha kabisa masuala ya muziki lakini baada ya mashabiki wengi kujitokeza wakimsihi kurudi, alikubali kuwa akimalizana na afya ya mama yake atarejea kwenye muziki na angalau kufanya wimbo mmoja wa kutoa shukrani kwa Mungu na mashabiki.

Mustafa vile vile alisema kuwa hayuko katika mahusiano ya kimapenzi baada ya kuachana na Notiflow miaka kadhaa iliyopita, na kusema kuwa huenda akarudi kwenye safu hiyo baada ya kujirudi kwani kwa asa hawezi kwa sababu alipoteza ujasiri wake kama mwanamume baada ya video ile ya kufanya kazi kwenye mjengo kuibua hisia mseto mitandaoni kumhusu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved