Mtangazaji Kamene Goro amewatupia kaa la moto watu waliodhani kuwa angeteseka na kuhangaika baada ya muda wake katika kituo kimoja cha redio humu nchini kukamilika.
Mrembo huyo ambaye alifunga harusi mwezi Aprili na mpenzi wake DJ Bonez kupitia Instagram yake aliwapa makavu wote waliojaaa kwenye kurasa zake wakimcheka na kumdhihaki baada ya kutangaza kuondoka redioni.
Kamene katika chapisho lake la kishari, aliwacheka wote waliokuwa wakisubiria kumuona akihangaika na kusema kuwa si shani yake kuteseka.
“Samahani kwa kutokuhangaika vile mlikuwa mnataka mimi niteseke. Sio sehemu yangu.....” Mrembo huyo aliandika kwenye chapisho lake jipya.
Tangu kuondoka redioni takribani miezi miwili iliyopita, Kamene amekuwa akishirikiana na mpenzi wake DJ Bonez katika kuongoza tafrija kwenye vilabu vya starehe haswa katika ukanda wa Pwani ya Kenya.
Mwezi Aprili, Kamene na Bonez walifunga harusi ya faragha ambayo ilihudhuriwa na marafiki zake wachache akiwemo Jalang’o ambaye alivujisha picha kutoka kwa tukio hilo.
Hata hivyo, wanamitandao hawakukosa la kusema na walianza kumshambulia mtangazaji huyo wakisema kuwa aliendea mwanamume ambaye si hadhi yake, wengine hadi wakisema kuwa ni yeye alikuwa anasimamia gharama zote za harusi hadi fungate.