logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zari afichua sababu ya kususia White Party ya Birmingham, UK licha ya kufika mapema

Zari alikuwa anatarajiwa kutokea kama mgeni wa heshima kwenye tafrija hiyo.

image
na Davis Ojiambo

Burudani26 June 2023 - 08:49

Muhtasari


  • • Zari alionekana akiwa anajivinjari kwa picha na mumewe Shakib Cham na kusema kuwa hakuna vile angejishusha na kujitokeza licha ya promota kugomba kufikia matakwa yake.
Zari ataja sababu za kususia White Party.

Mwanasosholaiti Zari Hassan amefichua sababu zilizomfanya kususia kutokea katika shoo ya Birmingham huko Uingereza ambapo alikuwa anatarajiwa kutokea wikendi iliyopita.

 Zari ambaye amekuwa akiipiga debe shoo hiyo alitarajiwa kuonekana Wikendi iliyopita na alisafiri hadi nchini Uingereza lakini hakuweza kutokea kama ilivyopangwa na sasa ametoa maelezo kwa mashabiki wake ambao aliwafeli kwa kutotokea.

Kwa mujibu wa mjasiriamalai huyo mkubwa mwenye makaazi yake nchini Afrika Kusini, alisalia tu kwenye chumba chake cha hotelini baada ya promota wa shoo hiyo kukosa kuafikiana na matakwa yake.

“Radhi zangu kwa kila mtu ambaye alitokea jana kwenye White Party ya Birmingham kuniona lakini hawakuweza kuniona. Kwa bahati mbaya, promota hakuweza kuafikia na matakwa yangu ya kimkataba na nimehisi kutamauka kama kila mtu kwa sababu nilikuwa nimeketi kwenye chumba change cha hoteli nikisubiri baada ya ahadi nyingi, haikutokea,” Zari aliandika kwenye Instastory yake.

Zari alionekana akiwa anajivinjari kwa picha na mumewe Shakib Cham na kusema kuwa hakuna vile angejishusha na kujitokeza licha ya promota kugomba kufikia matakwa yake.

Hata hivyo, aliwaahidi mashabiki wake kuwa wakati mwingine wataweza kumuona wakati promota ataweza kupanga na kuafikia na kila kipengele katika mkataba wake.

Ikumbukwe Zari ni mmoja kati ya wanawake maarufu barani Afrika na alijumuishwa kweney kipindi cha uhalisia cha Young, Famous & African kupitia mtandao wa Netflix ambacho kilikuwa kinawajumuisha vijana wenye utajiri mkubwa lakini pia na umaarufu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved