logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kisumu: Eric Omondi kumlipia matibabu ya tineja aliyepigwa risasi 9 kwa maandamano

Eric Omondi ameahidi kumlipia karo ya shule na kumjengea nyumba kijana anyedaiwa kupigwa risasi nane na polisi.

image
na Davis Ojiambo

Burudani25 July 2023 - 05:54

Muhtasari


  • • Eric alimtembelea kijana huyo katika hospitali ya Jaramogi mjini Kisumu alipokuwa amelazwa na kuahidi kumchangia kijana huyo zaidi ya shilingi milioni mbili.
  • • Kufikia saa 7:52 asubuhi ya leo Eric alitangaza alikuwa tayari ashachanga shilingi takriban 755,000.
Eric Omondi ata gaza nia ya kujiingiza katika siasa.

Mchekeshaji maarufu Eric Omondi ameahidi kumlipia karo ya shule na kumjengea nyumba kijana anyedaiwa kupigwa risasi nane na polisi wakati wa maandamano yaliyoandaliwa na muungano wa Azimio la Umoja.

Katika chapisho kwenye akaunti yake ya Instagram, Eric alimtembelea kijana huyo katika hospitali ya Jaramogi mjini Kisumu alipokuwa amelazwa na kuahidi kumchangia kijana huyo zaidi ya shilingi milioni mbili.

"Leo nimetembelea hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga na nikazungumza na majeruhi 18 wa ghasia iliyoshuhudiwa wakati wa maandamano lakini kijana mmoja alinishangaza sana. Jina lake ni Fidel Castro mwenye umri wa miaka 17. Alipigiwa risasi nane na bado yupo hai. Tutaungana kama Wakenya na kumchangia ili tuhakikishe maisha yake yatabadilika kabisa."

Mcheshi huyo ambaye sasa amegeuka na kuwa mtetezi wa haki za wanyonge nchini, aliendeleza ahadi zake kwa familia hiyo na kongeza kuwa atamjengea mama ya kijana huyo nyumba na kumfungulia biashara.

"Tutachanga pesa za kutosha kumlipia bili ya hospitali, tumjengee nyumba na kumfungulia yeye na watoto wake wanne biashara."

Kufikia saa 7:52 asubuhi ya leo Eric alitangaza alikuwa tayari ashachanga shilingi takriban 755,000 na kuendela kuwasihi Wakenya kuungana naye katika safari hii ya kubadilisha maisha ya familia ya Fidel.

Kulingana na taarifa ya kijana huyo, polisi walimfiatulia risasi 9 katika mgongo wake baada ya polisi kumvamia akiwa nyumbani kwao akicheza kadi na rafiki zake katika eneo la Nyamasaria, kaunti ya Kisumu.

"Alinipiga kwa mgongo , akarudia tena. Alikuwa anataka nianguke chini. Walinipiga risasi tisa kwa mgongo. Kusema ukweli naskia vibaya sana na langu tu ni naomba mnisaidie nipate haki."

Wiki iliyopita, mcheshi huyo aliweka harambee ya kumchangia Bw Victor Juma ambaye alikamatwa kwa njia isiyo ya kawaida siku ya Jumatano na afisa wa polisi aliyekuwa amevalia nguo za kawaida ambaye alijifanya mwandishi wa habari ili kuwakamata waandamanaji katika eneo la Mathare, Kaunti ya Nairobi.

Erci aliweza kufikisha shilingi 400,000 katika harambee hiyo aliyofanya kwenye akaunti yake ya Instagram na Facebook.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved