Mwanamuziki tajika, Sanaipei Tande amewashauri wanawake kuhakikisha wanatafuta hea kwanza na kupata mali kabla ya kuolewa.
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 38 ambaye awali alikuwa amesema hakuwa na haraka kuingia kwenye ndoa, alieleza kuwa wanawake wengi hufanya makosa wanapokimbilia kuolewa bila kumiliki kitu chochote.
"Kupata kazi ni muhimu sana kwa mwanamke. Endelea kufanya kazi kama una kazi inayolipa vizuri. Tumeshuhudia wanawake wengi wakiondoka kwenye ndoa wanakosa pesa za kujikimu."
Sanaipei aliongeza: "IKiwa mume wako anataka kukutunza ama kukupa pesa, bado unahitaji kuwa na pesa zako mwenyewe kwani huezi kutabiri kesho itakuwa aje."
Mwanamuziki huyo ambaye pia ni muigizaji katika mahojiano ya awali alisema kwamba hakuwa na haraka kuingia katika ndoa licha ya shinikizo kutoka kwa mashabiki wake kutaka atangaze mahusiano yake.
"Ndoa sio lengo kuu maishani acha iwe wazi kabisa. Nadhani ninapata mengi kutoka kwa mashabiki na kauli zao zinafanana oh unapaswa kuolewa sasa wewe ni mzee na inasikitisha, inanisikitisha kwa sababu najiuliza is that everything you think of?"
Katika mahojiano hayo hayo, alisema kuwa ndoa sio ishara mafanikio maishani. Hata hivyo alieleza kwamba angependa kupata watoto wawili pekee atakapo funga ndoa.
"Je, umesikia kwamba ikiwa haujaolewa kuwa haujafanikiwa? Inasikitisha sana. Tena ndoa sio lengo langu kuu lakini itakuwa vizuri kuolewa kuwa na mtu wa kunitunza kwa sababu, nasikia bwana ni mtoto wa kwanza wa mwanamke. Ninataka kuwa mama wa watoto wawili."