Marioo, msanii wa Bongo Fleva anayefanya vizuri Zaidi na ujio wa muziki wa Amapiano kwa mara ya kwanza amezungumzia madai yaliyoibuliwa mitandaoni kwamba mpenzi wake Paula wa Kajala aliharibikiwa na ujauzito.
Katika mahojaino kwenye runinga ya Wasafi, Marioo alionekana kukwepa swali hilo lakini pia hakuweza kusema ukweli kama Paula ana mimba yake.
“Msisikilize hayo maneno, nafikiri tuachane na hilo kwanza. Mama [Paula] yuko mjini na mtarajie tu kumuona, lakini hayo masuala ya kuharibikiwa kwa mimba mimi sijui lakini pia hapo kwa swali na kuwa na mimba tuombe Mungu tuseme Inshallah,” Marioo alisema watangazaji walipotaka kumdadisi kwa undani.
Msanii huyo baadae alifunguka akisema kwamba hayuko tayari kuzungumzia suala lilalomhusisha mpenzi wake Paula kwenye mahojiano hayo.
“Kusema ukweli kabisa, ukweli wangu kutoka Moyoni siko tayari kuzungumzia masuala kama hayo. Wakati mwingine tutaonana huko na tutazungumzia hilo, lakini tuseme inshallah,” alisema.
Msanii huyo alisema kwamba ila yeye angependa sana kuwa na mtoto bila kuchagua jinsia na pia kusema Paula yuko tayari kubadili dini kutoka Ukristo na kuwa Muislamu.
Kauli ya Marioo inakuja siku chache baada ya Paula kupitia ukurasa wake wa Snapchat kuachia kauli iliyoonekana kutowaamini wanaume tena akisema kwamba hawatofika mbinguni.
“Mbinguni sipajui sana ila ninaweza sema wanaume hawatafika kule,” Paula alisema.
Uhusiano wa Paula na Marioo uligunduliwa miezi michache iliyopita ulipoanza kama mzaha wengi wakihisi Marioo alikuwa anamtumia binti huyo wa muigizaji mkongwe Fridah Kajala kama vixen kweney wimbo wake.
Lakini waliendelea kugandana kama ruba na hata Kajaa mwenyewe kutia kidole kwenye uhusiano wao, akimtambua Marioo kama mkwe wake pika pakua.
Baadae ulikuja uvumi kwamba tayari Paula ameshajipa kwa Marioo na kumbebea kijusi, uvumi ambao haukuthibitika na baadae ukafuatwa na huo wa kudai kwamba imba imeshaharibika.