Mwanaharakati Boniface Mwangi amezipigia debe korosho akisema kwamba ni suluhu ya kudumu kwa wanaosumbuliwa na tatizo la kukosa nguvu za kiume.
Mwangi alipakia klipu ya video kwenye Facebook yake akiwa ndani ya gari huku mkononi amejihami na kiroba cha korosho.
Kwa maongezi na watu wengine ndani ya hilo gari, ni Dhahiri kufichua kwamba Mwangi alikuwa katika moja ya miji ya Pwani ambapo alipata bahati ya kupatiwa korosho.
“Kula korosho usitie vidole ndani, unajimwagie. Unasikia utamu ukiburunyaburunya. Unapata nguvu za kiume. Najimwagia mingi kwa kiganja kwa sababu nataka kuwa na utamu mwingi. Na ukila ukienda pale kumwaga unafanya hivyo kwa wingi sana,” Boniface Mwangi aliwaambia abiria wenzake ndani ya hilo gari.
Mwangi alitumia fursa hiyo kuwaomba mashabiki wake kumfuata pale katika mtandao wa TikTok akisema kuwa amejaajaa pale.
Alisema kuwa akiwa Mombasa, ilimbidi kuboresha Kiswahili chake kwa lafudhi ya pwani ili asije akaonekana mshamba wa bara.
“Utamu wa korosho muulize mpokeaji yule unaenda kumpa. Mimi naitwa Suleiman sasa. Hapa natongoza lugha tu, ndio wanasema kwamba dera bila makalio ni kanzu. Kwa hivyo kama huna makalio usivae dera,” alisema kwa vichekesho.