In Summary

• "CV napokea kwa makosa ya uchapaji na sarufi ya uzembe na ni kama kwanini?" - Kamene.

• Aliwashauri watu kurudia kusoma ili kutoa makosa ambayo yanaweza kuepukika.

Kamene Goro.
Image: Instagram

Mtangazaji Kamene Goro ameonesho kero lake kwa watu wazima walio na umri wa miaka 30 kwenda mbele ambao bado wanapata taabu kutofautisha silabi kati ya maneno ya Kiingereza ambayo yanatamkika kwa sauti sawa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kamene Goro alisema kuwa amelazimika kulizungumzia hilo baada ya kuona makosa ya kawaida kama hayo kwenye CV za watu wengi ambazo anazipokea.

Goro alisema kuwa makosa hayo mengi ambayo yanapuuzwa na watu mwishowe huwanyima nafasi za kazi na hivyo kutathmini kuanzisha darasa la wakubwa ili kufunza watu kuhusu maneno ya Kiingereza, jinsi yanaandikwa na kutamkwa.

“Ninaangalia tahajia mbaya ya watu na sarufi nikifikiri labda nianzishe darasa la tahajia na sarufi msingi. Vipi uko zaidi ya [miaka] 30 na bado huwezi kutofautisha kati ya This na These na Their hata There, bado ni tatizo jamani?" Kamene alishangaa.

Aliwataka wanaomchukulia vibaya kusikiliza maana yake na kudai kwamba pengine ni uzembe unaofanya watu kuacha makosa ya tahajia kutokea bila hata kuonekana kuyarekebisha.

Aliwashauri watu haswa wanaolenga kuandika barua za kuomba kazi kupitia mara kadhaa ili kuondoka makosa hayo ya tahajia na pengine kuwapa wengine barua hizo kusoma kwa macho mapya.

"Angalia, msinielewe vibaya sio makosa ya sarufi yake mbaya na ukosefu wa mpango wa kuifanya iwe bora zaidi ambayo inanikera. Tunaishi katika zama ambazo ufikiaji wa habari ni bure na rahisi kwa hivyo huna kisingizio. CV napokea kwa makosa ya uchapaji na sarufi ya uzembe na ni kama kwanini? Angalia mara mbili mbili, itume kwa mtu aitazame kwa macho safi au hata fanya google kuwa rafiki yako. Unakosa fursa kwa uzembe. "

View Comments