Mwanasosholaiti mwenye ufanisi mkubwa wa nchini Kenya Vera Sidika amemtambulisha mpenzi wake mpya mwezi mmoja tu baada ya aliyekuwa mpenzi na baba wa watoto wake Brown Mauzo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sidika alipakia picha ya kijana huyo ambaye pia jina lake ni Brown.
“Nakupenda hadi milele mpenzi wangu G Brown. Mshikaji wangu katika uchizi nakupenda sana,” Vera Sidika aliandika akiambatanisha na picha ya jamaa huyo ambaye amepaka nywele rangi ya kahawia.
Katika picha nyingine, Sidika alipakia video ya jamaa huyo alicheza densi na kudokeza kwamba ni raia wa Jamaica.
“Wajamaika ndio kusema, mpenzi wangu G Brown,” aliandika.
Sidika ambaye yuko nchini Marekani kwa kusherehekea tafrija ya siku yake ya kuzaliwa aliamua kupakia picha ya jamaa huyo ikiwa ni wiki chache baada ya kutoa kidokezo kwa mashabiki wake kwa kupakia picha ambayo alikuwa ameifunika uso kwa kutumia emoji.
Mwishoni mwa mwezi Agosti, Brown Mauzo katika aya ndefu alieleza kwamba yeye na Vera Sidika si mtu na mpenzi wake tena.
Mauzo alisema kwamba waliafikia kutengana baada ya kuona kwamba penzi lao halingeweza kupata mwamko mpya tena kwani kila mmoja alikuwa ameshiba kumuona mwenzake.
Wawili hao wana watoto wawili pamoja, msichana na mvulana ambaye hajamaliza mwaka mmoja tangu alipozaliwa.
Kumtambulisha mpenzi mpya mwenye jina Brown kuliwazuzua mashabiki mitandaoni ambao baadhi walihisi kwamba mwanasosholaiti huyo anapenda sana watu wenye majina Brown.