Siwezi kubali urafiki au maogezi yafanyike wakati ninapotengana na mpenzi wangu urafiki huu hauna ladha ni wakupotezeana muda tu ni kauli yake muigizaji Wema Sepetu.
"Wakati unapoachana na mpenzi wako na ukaingia kwa mapenzi na mchumba mwingine jambo la kuzungumuza na Ex wako alifahi kamwe mkiachana kila mtu apambane na maisha yake mbila kumshirikisha mwingine",alisema.
Muigizaji huyu mashuhuri ambaye hivi majuzi alitunikiwa nafasi ya kuwa mmoja wa washauri wa maswala ya ndoa kwenye kituo cha Radio Furaha FM nchini Tanzania, alipinga mazoea ya kuzungumza na waliokuwa wachumba.
"Nini ambacho mnataka kuzungumza wakati mnapotengana kipi hicho hamkuweka wazi wakati mlipokuwa wachumba mimi siwezi hata kwa dakika moja kwa maana urafiki na Ex wako unaweza ukachangia uhusiano mwingine jambo ambalo litachangia mapenzi bandia.
Kwenye mjadala huu na wasikilizaji wake Wema aliwaonya kwa kile alikitaja kuwa kitachangia madharau na mzigo mzito ndani ya ndoa iwapo mtu yeyote atajishirikisha na urafiki wa kando na ex wake.