logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DJ wa Diamond kumpa Mbosso dili la matangazo ya waganga baada ya marufuku ya muziki

Mbosso alipigwa marufuku miezi 3 kutojihushisha na muziki.

image
na Davis Ojiambo

Burudani06 November 2023 - 08:58

Muhtasari


  • • Hili ni pigo kubwa kwa wasanii hao haswa Mbosso ambaye amekuwa akitamba na kufana pakubwa kwa kuigiza character ya Sele, katika moja ya wimbo wake.
Romy Jones na Mbosso

RJ the DJ, ama Romy Jones amejitokeza na kuonyesha kusikitishwa kwake na hali ya Mbosso baada ya kufungiwa na baraza la Sanaa Tanzania, BASATA kutojihusisha kwa kazi za Sanaa kwa kipindi cha miezi 3.

DJ huyo rasmi wa Diamond ambaye pia anatajwa kuwa kaka wa kufikia kwa msanii huyo tajiri alikwenda kwenye picha za Mbosso Instagram na kumwambia kwamab asife moyo kwani yeye kama rafiki mwema ana njia nyingine ya kumsaidia katika kipindi hiki ambapo hawezi tena kufanay shughuli yoyote inayohusiana na Sanaa katika ardhi ya Bongo.

Mbosso alipakia rundo la picha akiashiria kwamba adhabu hiyo imekuwa pigo kubwa kwake na hata kumpa msongo wa mawazo.

Hapo ndipo Romy Jones alimtania kwamba pengine akuwe akipakia video fupi za miziki yake kwenye mitandaoni kwani marufuku inajumuisha kutofanya shoo yoyote wala kuachilia miziki yoyote kwa kipindi cha miezi mitatu.

Jones anayejulikana kwa kufanya matangazo ya waganga na dawa za kiasili pia alimdokezea Mbosso kwamba yuko tayari kumpa dili hilo la kuwa mmoja wa wanaotumia mitandao yao kutangaza dawa za waganga, angalau kwa kipindi hiki ambacho hawezi fanya chochote cha maana kisanaa kwa kutumia akaunti zake mitandaoni.

ASAIVI LABDA UWE UNAJIPOSTIA ZAKO TU PICHA MWAYA AU NIKUPE MATANGAZO YA WAGANGA,” Romy Jones alimwandikia Mbosso.

Utakumbuka Awali tuliripoti kwamba Mbosso, Whozu na Billnass walipewa adhabu hiyo na BASATA baada ya video ya ngoma yao ya Ameyatimba Remix kutajwa kuwa inakiuka kanuni za kimaadili kwa kudhalilisha utu wa mwanamke.

Hili ni pigo kubwa kwa wasanii hao haswa Mbosso ambaye amekuwa akitamba na kufana pakubwa kwa kuigiza character ya Sele, katika moja ya wimbo wake.

Mbosso amekuwa akibuni njia tofauti za kuonesha Sele – jamaa wa hovyo mitaani ambaye anabugia bangi na pombe kucha kutwa – katika tamasha la Wasafi kwenye mikoa mbali mbali tangu Agosti.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved