In Summary

• Nabii kwenye alisema kuwa yeye ni tajiri na umri wake ni sawa na ule msanii wa injili Justina alitaka kuwa mchumba.

Nabii Mahewa na Justina Syokau
Image: Screengrab, Facebook

Siku chache baada ya msanii wa nyimbo za injili Justina Syokau kuonekana na bango akitafuta mchumba,mchungaji mmoja kwa jina Nabii Mahewa amejitokeza na kufunguka kuwa yuko tayari kumuoa.

Nabii kwenye alisema kuwa yeye ni tajiri na umri wake ni sawa na ule msanii wa injili Justina alitaka kuwa mchumba.

"Mimi ni tajiri,na utajiri wangu unafahamika na wengi jijini Mombasa nimeona ujumbe wa Justina mtandaoni, niko tayari kuchumbiana naye kwa maana ni mke mwema," Nabii alisema.

Mhubiri huyo chipukizi aliendelea kusema kuwa;

"Niko tayari kumzawadi kanisa langu moja ndiposa tuendeleze injili naye najua wakati alipokuwa jijini akitoa ujumbe ni mimi alitaka kwa maana niko na pesa na umri sawia,"alisema Nabii Mahewa.

Nabii alisema kuwa mwimbaji Justina alikuwa akimtumia jumbe kwenye mtandao wake wa instagram ili wachumbiane.

Kwenye mahojiano hayo nabii huyu aliendelea kutoa kauli zake akisema kuwa  walikuwa na mpango wa kukutana na Justina Syokau  kwa hoteli moja ili kujuana zaidi.

"Tumekubaliana kukutana nampenda Justina Syokau sana iwapo tutakubaliana kuchumbiana nitamtambulisha kwa washirika wangu ili tufunge ndoa msimu wa krismasi. Mungu amenionyesha kwa maono kuwa tutabarikiwa na wavulana wawili  iwapo tutaoana na mwimbaji Syokau," alisema.

 

View Comments