Msanii wa Tanzania, Revokatus Kipando, almaarufu Baba Levo, amemsifia Diamond Platnumz akimtaja kuwa 'Risk taker' mkubwa ambaye anawekeza kwa wasanii bila kujali kupoteza hela zake.
Baba levo alisema hayo wakati wa sherehe zilizoandaliwa na Lebo la Diamond Wasafi ili kumutambulisha msanii mpya kwenye Lebo.
"Diamond ni msanii wa kuigwa kwa mambo makuu anayoyafanya licha ya kuwa alipoteza hela nyingi baada ya kuwatambulisha wasanii na baada ya kung'aa wakajitoa kwa Lebo yake bado yuko na roho ya upendo kwa wasanii, ametumia hela nyingi ili kufanikisha nyota nyingi bila kujali kama hela zake zinapotea yeye anafanya hivyo kwa mapendeleo kwa sanaa",alisema.
Msanii huyo aliwashauri wasanii wote chini ya Lebo la Wasafi na wale wajiodoa baada ya kutajirika kumpa mwanzilishi wao heshima kwa kuwa alitumia hela nyingi kwa sababu ya mafanikio yao.
"Sidhani kuna mtu anaweza kuchukuwa hatua ya kuekeza mabilioni kwa wasanii bila kujali faida atakayopata kwake, Diamond amejaribu sana kuwa mfano bora,"alisema Baba Levo.