In Summary

• Pia alitania kwamba yeye ndiye rais na afisa mkuu wa mahusiano yaliyofeli lakini pia akakiri kwamba ladha yake anaitambua vizuri Nelly Oaks.

Akothee.
Image: Facebook

Msanii na mjasiriamali Esther Akothee amekanusha madai kwamba amekuwa akitupiana cheche za maneno na TikToker Nyako, akisema kwamba tiktoker huyo ndiye amekuwa akilivuta jina lake kwenye video zake katika mtandao huo wa TikTok.

Akothe kupitia kurasa zake mitandaoni alisema kwamba yeye hana muda wa kujibizana na wale aliowahita watu chipukizi katika mitandao ya kijamii, kwani ana mambo mengi ya kujishughulisha nayo.

“Nimekuwa nikisema mwaka mzima. Wanawake wanaovutiwa na maisha yangu wanapaswa kukubali kuwa ninawapa msukumo na Heshimu GOAT tu. Baadhi ya wanawake waliondoka Kenya kutafuta unafuu wa kimaisha. Waendelee na maisha yao na waache kuliburuza jina langu kwenye hustle zao za kila siku, siwafuati wala siwajui, niliacha kuhoji kwanini wanaendelea kuliburuza jina langu kwani niligundua mimi ndiye kigezo cha jinsi single mother wa mafanikio anavyotakiwa kuonekana. Sijamblock mtu yeyote kufanya kile anachoweza kufanya. Nilitengeneza chapa yangu na hadithi yangu ya mafanikio, sihitaji jina la mtu yeyote kwa umaarufu,” Akothee alisema.

Mjasiriamali huyo aliendelea kujisifia kwa wasifu mrefu akisema kwamba yeye ni mama mwenye nyumba asiyelipa kodi ya kila mwezi, mkurugenzi mkuu wa shule lakini pia mwandishi wa vitabu.

Pia alitania kwamba yeye ndiye rais na afisa mkuu wa mahusiano yaliyofeli lakini pia akakiri kwamba ladha yake anaitambua vizuri Nelly Oaks.

“Mhitimu mzima kama mimi nina shahada ya usimamizi wa biashara, kufanya biashara kote nchini. Super star, rais wa single mothers, nina watoto wenye nidhamu wenye shahada, Mkurugenzi mzima wa AKOTHEE ACADEMY, Rais wa AKOTHEE FOUNDATION. Mkurugenzi Mtendaji, gwiji namba moja wa masoko, Esther Mwandishi, Afisa mkuu wa mahusiano yaliyofeli 🤣🤣, Mpangaji mkuu wa jinsi maisha yanavyoonekana katika uhalisia, Nyota aliyeshinda tuzo duniani, tomato ya Nellyoaks… Hutanipata katika ubadilishanaji wa maneno machafu wa mtandaoni na watoto chipukizi,” aliongeza.

Akothee aliwataka wanawake wote wanaomchamba akisema kwamba ni wakati sasa wajikusanye na kutafuta kitu cha kufanya ili angalau kufikia nusu ya mafanikio yake badala ya kumtupia maneno mitandaoni.

“Watu waamke tu watafute kazi za kufanya. kukusanya maisha yao waliotawanyika kukubali na kuendelea. Sote tuna nguvu tofauti, asili tofauti na marudio tofauti, hatushiriki Hakuna chochote kwa pamoja,” alisema.

View Comments