logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Siwezi umia Rayvanny akitoka kimapenzi na mrembo mwingine - Fahyvanny

Angekuwa hana hizo skendo ningekuwa hata na mimi nasema ‘eeh huyu mwanamume vipi.

image
na Davis Ojiambo

Burudani21 November 2023 - 07:49

Muhtasari


  • • “Sasa wewe mwanamume wangu, ukiniambia eti ndio anamfanya mtu Fulani unadhani ndio unaniumiza au?" Fahyma aliuliza.
  • • Alisema kwamba skendo za kutoka kimapenzi za Rayvanny ndizo huonesha kwamba kweli ni mwanamume kamili.
Rayvanny na Fahyvanny.

Mrembo Fahyvanny amefichua kwamba hawezi umia wala kuvunjika moyo iwapo mpenzi wake, Rayvanny ataamua kutoka kimapenzi na mrembo mwingine.

Fahyma ambaye alikwenda live kwenye Instagram yake, alisema kwamab wale wanaofikiria kuwa yeye ataumia kwa kujua Rayvanny aliwahi kutoka kimapenzi na mrembo mwingine wanaharibu muda wao tu, akisema kwamba kitendo cha Rayvanny ku’cheat kwake ni kawaida tu sawa na kusaidiwa.

“Sasa wewe mwanamume wangu, ukiniambia eti ndio anamfanya mtu Fulani unadhani ndio unaniumiza au? Wala siumii, nasaidiwa mimi,” Fahyvanny alisema.

Mama huyo wa mtoto mmoja ambaye wamerudiana na Rayvanny mwezi Machi mwaka huu alisema kwamba kinachomfanya kutoumia ni hakikisho alilolipata kutoka kwa Rayvanny kwamba yeye ndiye mwanamke mzuri na wa ndoto za msanii huyo kutoka Next Level Music.

Alisema kwamba skendo za kutoka kimapenzi za Rayvanny ndizo huonesha kwamba kweli ni mwanamume kamili.

“Maana mimi ndio the best wife in town, halafu yule mwanamume ni lijali, na angekuwa hana hizo skendo ningekuwa hata na mimi nasema ‘eeh huyu mwanamume mbona sisikii’ ningekuwa nasema ‘vipi huyu’ lakini yuko vizuri, namuamini, acha atembeze kichapo. Hata akitoa laki 5 kwa one-night stand sio mbaya. Halafu akimaliza anarudi kwa mke wake hapa anatoa milioni 10,” alisema Fahyma.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved