Muigizaji Sandra Dacha ameibuka na utafiti binafsi kwamba idadi kubwa ya wanawake waliotoroka ndoa zao kwa sababu za kuwa na wanaume fisi ndio wengi wanaonyemelea ndoa za wanawake wenzao.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Dacha anayejitambua kwa jina ‘Biggest Machine’ kutokana na umbile la mwili wake alidai kwamba hadi asilimia 80 ya wanawake walioomba talaka katika ndoa zao kwa sababu ya kugundua wanaume wao wana’cheat nje ya ndoa, sasa hivi wanawake hao ndio wanaotoka kimapenzi na wanaume walioko katika ndoa bila kujali kwamba pia kwao hiyo ni ku’cheat.
“Asilimia 80 ya wanawake walioachika wanachumbiana na wanaume walio katika ndoa LAKINI waliachana kwa sababu ya mwanaume aliyecheat,” Dacha alisema.
Tamko hilo la Dacha lilionekana kuwa la kawaida lakini lilifungulia mirija ya maoni kutoka kwa mashabiki wake, baadhi wakidai kwamba hiyo ndio njia pekee ya wanawake kulipa kisasi na wengine wakiitaja hatua hiyo kuwa ya kipumbavu.
Haya hapa ni baadhi ya maoni;
“Na inaitwa upumbavu, bora uwe na mumeo na wewe pia ucheat bora uko katika ndoa yako,” Joy Jaber alisema.
“Tuseme wanalipa kisasi au? Inamaanisha kuwa wanahimiza maovu ambayo wanachukia sana,” Samson Solomon alisema.
“Ndiyo. Walisalitiwa kimapenzi kwa hiyo ni unifanyie hivyo na mimi nikufanyie hivyo sitaki kujua ni bwanake nani nyako,” Lyndsey Odero.