logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mandonga atangaza kuwa tayari kupigana ngumi na Harmonize

Katika siku za hivi karibuni, Harmonize na Mwakinyo wamekuwa wakitupiana mikwara

image
na Davis Ojiambo

Burudani29 March 2024 - 06:11

Muhtasari


  • • “Mimi Mandonga mtu kazi nililipokea hilo vizuri kwa maana mchezo huu ndio kazi yetu, kwa hiyo mimi niko tayari, ni yeye atupange tarehe tu,” Mandonga alisema.
Mandonga na Harmonize

Bondia mwenye vituko na ucheshi mwingi kutokea Tanzania, Karim Mandonga maarufu ‘Mtu Kazi’ ameweka wazi kwamba yuko tayari kupigana ngumi na msanii Harmonize.

 Hii ni baada ya Harmonize kutangaza kwamba ushindani kwenye muziki umepungua na yuko tayari kuzichapa dhidi ya bondia Hassan Mwakinyo.

Katika siku za hivi karibuni, Harmonize na Mwakinyo wamekuwa wakitupiana mikwara mitandaoni, huku Harmonize akimuomya bondia huyo kwamba atambomoa na kufanya mchezo wa ngumi kuharamishwa nchini humo.

Hata hivyo, akuzungumza na media moja, Mandonga alisema kwamba yuko tayari muda wowote kupigana na Harmonize, na ni juu ya msanii huyo wa Konde Gang kupanga tarehe tu.

“Mimi Mandonga mtu kazi nililipokea hilo vizuri kwa maana mchezo huu ndio kazi yetu, kwa hiyo mimi niko tayari, ni yeye atupange tarehe tu,” Mandonga alisema.

Bondia huyo kwa kujishasha alisema kwamba hata hataki hela za Harmonize, dola laki moja ambayo alitangaza kuweka kama dau, bali anachotaka ni kumpiga tu ili atulie.

“Unajua mimi nishakuwa bondia wa kitaaluma, ila mwambie hela sitaki mimi, hela zake achukue yeye mimi ninachotaka nimpige tu ili atulie. Si anasema yeye ni tembo, mimi nataka nimkate mkonga, mwambie Mandonga mtu kazi sina shida yoyote, ninachotaka nimpige tu ili atulie,” Mandonga alisisitiza.

Harmonize amekuwa akitaniana na wanabondia wa Tanzania akisema kwamba yeye ni mbaya sana katika kumpiga ndio maana alishawahi jiwekea nadhiri kwamba hatoweka mkono wake kwa mwili wa mtu yeyote lakini kwa bondia hao inabidi avunje yamini yake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved