logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kartelo atangaza kuondoka Chipukeezy Show inayopeperushwa runingani KBC, baada ya misimu 3

“Woza, baada ya misimu mitatu yenye ufanisi nikiwa miongoni mwa Chipukeezy Show," aisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani31 March 2024 - 10:10

Muhtasari


  • • Mkuza maudhui huyo aidha aliorodhesha baadhi ya majukumu ambayo amekuwa akitekeleza katika shoo hiyo inayoongozwa na MC wa rais – Chipukeezy.
CHIPUKEEZY NA KARTELO

Kartelo ambaye ni mcheshi maarufu wa Kenya, mwimbaji, mtangazaji wa vyombo vya habari na mkuza maudhui wa mitandaoni ametangaza kuondoka katika shoo ya mchekeshaji Chipukeezy baada ya misimu 3.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kartelo aliweka wazi kwamba mwisho kwake katika Chipukeezy Show ambaye imekuwa iipeperushwa kwenye runinga ya KBC umefika na kuwashukuru watu wote akiwemo Chipukeezy kwa kushirikiana kwa miaka 3 iliyopita.

“Woza, baada ya misimu mitatu yenye ufanisi nikiwa miongoni mwa Chipukeezy Show, ninatangaza kuondoka kwangu,” taarifa hiyo kupitia Instagram yake ilisoma.

Mkuza maudhui huyo aidha aliorodhesha baadhi ya majukumu ambayo amekuwa akitekeleza katika shoo hiyo inayoongozwa na MC wa rais – Chipukeezy.

“Kukuletea hadithi, utambuzi na burudani katika nyumba yako kumekuwa heshima kubwa isiyoweza kuelezeka kwa maneno. Huku nikipiga hatua kwenda kwa ukurasa mwingine, ningependa kueleza shukrani zangu kwa sapoti na uaminifu kutoka kwa mashabiki, washikadau na timu nzima,” ilisomeka kwa ukamilifu taarifa hiyo.

Miaka miwili iliyopita baada ya kile kilitajwa kuwa ni bifu baina yao, wawili hao walitangaza tena kurudi pamoja na kuja na shoo hiyo.

Wawili hao walikuwa marafiki wa kufa kuzikana tangu miaka ya nyuma mbapo walikuwa na shoo ya ucheshi ambayo ilikuwa inapeperushwa katika vituo vya runinga za Ebru na TV47 ila baada ya janga la Korona mwaka 2021 walisemekana kukosana vibaya hata kutopigiana simu wala kushabikiana kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya shinikizo kutoka kwa mashabiki wao wakitaka warudiane, Oktoba 2022,  Chipukeezy kupitia Instagram yake alidokeza kurudi kwa shoo hiyo yake na kumtaja Kartelo kama mmoja wa watu watakaoianzisha upya kama ilivyo kuwa awali.

“Kurudi kwa shoo ya Chipukeezy, uko tayari Kartelo?” Chipuukeezy aliandika.

Vile vile, Kartelo ambaye mara nyingi hupenda kutumia lugha ya mitaani almaarufu Sheng alipakia picha yao ya pamoja enzi za nyuma na kusema shoo hiyo inasubiriwa sana kwenye runinga.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved