logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Mimi ni Mluhya ninamiliki ‘kisiagi’ hautalala njaa!” – Jamaa ambembeleza Nyako kumpenda

“Nyako ninataka kukuoa, mimi ni Mluhya ," jamaa huyo alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani31 March 2024 - 07:49

Muhtasari


  • • “Nyako ninataka kukuoa, mimi ni Mluhya ninamiliki posho-mill hivyo hautalala njaa,” sehemu ya ujumbe kwenye bango lake ulisoma.
Nyako

Mwanamume mmoja kutoka sehemu za Magharibi mwa Kenya amechukua kwenye mtandao wa TikTok akiweka msururu wa picha zake kwenye muundo wa video bango la kumtongoza tiktoker Nyako Pilot.

Kijana huyo kwa jina Ainea Nabwera alionekana akiwa ameshikilia bango lenye ujumbe uliokusudiwa kumfikia TikToker huyo ambaye anaishi Ujerumani.

Nabweri katika ujumbe wake wa kumtupia ndoana ya mapenzi Nyako, alimhakikisha kwamba pindi atakapompenda basi ajue kwamba hajafanya uamuzi mbaya kwani hakuna siku atawahi lala njaa wakiwa wapenzi.

Nabweri alisema kwamba kwa kumhakikishia hilo, mwanzo Nyako ajue kwamba yeye ni mmiliki wa mashine ya kusiaga mahindi na kutengeneza nafaka kwa lugha ya mtaani ‘kisiagi’ jambo ambalo litahakikisha unga unapatikana kwake muda wote saa ishirini na nne kwa wiki.

“Nyako ninataka kukuoa, mimi ni Mluhya ninamiliki posho-mill hivyo hautalala njaa,” sehemu ya ujumbe kwenye bango lake ulisoma.

Hata hivyo, mpaka wakati taarifa hii ilikuwa inachapishwa, Nyako hakuwa ametoa jibu kwa kijana huyo lakini baadhi ya watumizi wa TikTok walikuwa na haya ya kusema;

“Nyako akijibu niitwe ndio nijuwe kma ndacommet ama hapana 😂😂 anyway all the best braza,” Nzish Mkisa.

“Wacha Nyako aone hii, comeback utapata utatii kaka,” Mama Leon2019.

“Wewe unajitafutia shinda tena kwa bei nafuu kabisa,” Prossy.

Katika video hiyo, kijana huyo aliiambatanisha na wimbo wa ‘Salima’ wake Linex Sunday aliomshirikisha Diamond Platnumz mwaka 2015.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved