logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Nikiwa mlevi huwa sijui kilichotokea siku iliyopita, naisikitikia nafsi yangu” – Magix Enga

“Wewe huelewi nakunywa juu ya stress,” Enga alimjibu.

image
na Davis Ojiambo

Burudani18 July 2024 - 12:41

Muhtasari


  • • Akionekana kufagilia sababu yake ya kulewa, Enga alisema kwamba anakunywa kwa sababu anawapenda mashabiki wake ambao wengi wanamjua licha ya yeye kutowajua.
MAGIX ENGA

Msanii na mzalishaji wa muziki Magix Enga kwa mara nyingine ametoa taarifa za kutilia mashaka kuhusu hali yake, na mihangaiko dhidi ya uraibu wa vilevi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Magix Enga anadai kwamba amerudi kwenye unywaji wa pombe kutokana na kile alimjibu mmoja akisema ni msongo wa mawazo.

Enga, ambaye aliokolewa awali kutoka maisha ya mihangaiko na kupelekwa katika kituo cha kurekebisha tabia na baadae kutafutiwa ajira ya kuzaisha miziki katika studio moja mjini Eldoret amekuwa akikiri katika machapisho yake hivi majuzi kwamba amerejelea katika uraibu huo.

Akionekana kufagilia sababu yake ya kulewa, Enga alisema kwamba anakunywa kwa sababu anawapenda mashabiki wake ambao wengi wanamjua licha ya yeye kutowajua.

“So sad sijui watu but wananijua sana because of my music so I drink every day because I love my fans and am always too good to everyone which I find it crazy kuongea na mtu anakujua na mimi simjui,” Magix Enga alisema.

Mzalishaji huyo aliisikitikia nafsi yake akisema kwamba kila mara anaomba Mungu kumsaidia kwani wakati amelewa, huwa anapoteza kumbukumbu zote na hawezi kujua ni kipi kilichojiri siku iliyopita.

“Mungu anilinde na vile mimi hulewa nikilia nakuongea vitu sijui, Nikiwa mlevi don’t call me please. Ata sijuangi kilichotokea siku iliyopita 😭 Najisikitikia nafsi yangu,” Enga aliongeza.

Hata hivyo, mmoja alijaribu kumshauri kurudi kanisani kumtafuta Mungu, jambo ambalo Enga alionekana akipinga na kusema kwamba matatizo yake ni kutokana na stress.

“Kusudia kwenda kanisani. Nenda tu pale na usikilize neno moja au mawili. Iyo pesa mingi unakunywa peleka watoto home watasaidika sana. Hakuna mtu anakuja kukuokoa nigga, lazima iwe wewe na wewe peke yako,” mmoja alijaribu kumpa ushauri.

“Wewe huelewi nakunywa juu ya stress,” Enga alimjibu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved