logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zuwena wa Diamond akiri kumpenda Bunny Asila, wiki baada ya kusema hawezi date Mkenya

“Mimi siwezi kuwa na mwanamume wa Kenya, kwa Kiswahi chao kile…” alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani06 August 2024 - 09:31

Muhtasari


  • • “Unaujua Wakenya wana hela halafu wanajielewa sana. Ni hivyo halafu pia mimi nampenda sana Bunny Asila. " alisema.
ZUWENA WA DIAMOND AKIRI KUMPENDA BUNNY ASILA.

Vixen wa video wa msanii Dimaond Platnumz kwenye wimbo wa Zuwena, Recho Elias maarufu ‘Zuwena wa Diamond’ ameibuka na mada mapya akionesha nia yake ya kuchumbiana na msanii wa injili wa Kenya Bunny Asila.

Katika mahojiano, Zuwena awali alikuwa amekula yamini kwamba hawezi jikuta ametoka kimapenzi na mwanamume yeyote kutoka Kenya akidai kwamba Kiswahili cha Wakenya kinakera na kuudhi.

“Mimi siwezi kuwa na mwanamume wa Kenya, kwa Kiswahi chao kile…” alisema akidai kuwa matamshi ya wanaume wa Kenya ni kama ya kufokea mtu bila hata chembe ya mahaba ndani yake.

Kauli hii iliwaudhi baadhi ya Wakenya ambao walimzomea vikali wakimtaka kuwaomba wanaume wa Kenya radhi.

Katika video nyingine, mrembo huyo alionekana kujutia kauli yake hiyo akisema kwamba anawakubali wanaume wa Kenya kwa vile ni wachapakazi na wenye hela.

Aidha, alisema kwamba akipata nafasi ya kuchumbia mwanamume wa Kenya basi bila kupepesa jicho ataudondosha moyo wake wa mapenzi kwa msanii Bunny Asila ambaye anaishi zake Ufini.

Pia alitumia fursa hiyo kuwaomba radhi Wakenya kwa kauli zake zilizowachafua roho.

“Unaujua Wakenya wana hela halafu wanajielewa sana. Ni hivyo halafu pia mimi nampenda sana Bunny Asila. Unajua Bunny Asila kwanza vile alivyo yaani ni handsom boy Fulani na nashukuru amenipenda mimi na mimi nampenda, ni kijana Fulani hivi ambaye yuko romantic,” alisema

“ Na mimi ninachoomba kikubwa kwa ndugu zangu Wakenya, mimi ni familia yenu ila kama nimewakosea sikumaanisha kuwakosea kihivyo ila ilikuwa tu ni hasira tu, naomba mnisamehe nawapenda sana Wakenya,” aliongeza.

Hata hivyo, Bunny Asila angali bado kuvunja kimya chake kuhusu nia ya Zuwena kutoka kimapenzi naye.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved