logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Mungu alinipa nafasi nyingine tena” – Kenyan Prince baada ya kuhusika katika ajali nyingine

Kijana huyo alimshukuru Mungu akisema kwamba alipewa nafasi nyingine adimu ya kuishi.

image
na Davis Ojiambo

Burudani07 August 2024 - 13:58

Muhtasari


    KENYAN PRINCE.

    Mfanyibiashara wa ubadilishanaji wa sarafu, Kenyan Prince amehusika kaitka ajali nyingine, wiki chache baada ya kunusurika ajali nyingine tena.

    Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kenyan Prince alichapisha video na picha za mabaki ya gari alilokuwa akisafiria pamoja na marafiki zake wakati ajali ilipotokea.

    Kijana huyo mkwasi alifichua kwamba japo gari liliharibika vibaya kutokana na athari ya ajali hiyo, yeye na marafiki zake wako katika hali shwari na wanaendelea kugangwa hospitalini.

    Kijana huyo alimshukuru Mungu akisema kwamba alipewa nafasi nyingine adimu ya kuishi.

    “Usiku mbaya ulioje! Dereva wangu, marafiki na mimi tunaendelea kupata matibabu hospitalini, ahsante sana kwa wale wote wamenisikitikia, nitarejea kwenu na taarifa. Mungu alinipa nafasi nyingine tena,” Kenyan Prince aliandika.

    Aidha, kijana huyo alidokeza kwamba kuna mama ambaye alimtabiria kupata ajali ya kifo, akimshukuru Mungu kwa kutokubali utairi huo kutimia.

    “Yule mama alisema atanifanyia kitu gari liniinue miguu, enyewe halali, Mungu yupo bado niko hai. Tutajaribu tena kesho,” aliongeza.

    Mnamo Julai, Kenyan Prince alihusika katika ajali ya gari akiwa na Mercedes benzgle yake Siku Moja Baada ya Audi TT yake Kuhusika Katika Ajali Nyingine.

    Ajali ya kwanza ilihusisha gari lake na mwendesha bodaboda. Kulingana na mfanyabiashara wa Forex, Audi iligonga mapema na ikapoteza udhibiti. Tukio hili sio tu lilisababisha mtafaruku lakini pia lilienea haraka na kuwa hali ya karibu ya uharibifu.


    RADIO JAMBO FREQUENCIES

    Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


    logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved