In Summary

• Kutokana na ukweli huo machoni pake, Jabidii alisema alihisi kabisa muziki ni utapeli na hata akawaza kuachana nao.

Jabidii
Image: Hisani

Msanii wa injili ya kisasi kipya humu nchini, Jabidii amefichua jinsi alihisi kukata tamaa ya kufanya muziki baada ya Mapato duni ya mirabaha.

Akizungumza na Dr Ofweneke kwenye runinga ya TV47, Jabidii alifichua kwamba alipata mirabaha ya shilingi eldu 2 pekee kutoka kwa ngoma yake ya kwanza ku'hit, Odi Dance.

Msanii huyo alisema alijihisi vibaya kupokea kiasi hicho kidogo kutoka kwa mamlaka inayosimamia hakimiliki za kazi za Sanaa, kwani kupindi hicho wimbo huo ulikuwa maarufu kila mahali na zaidi ya yote kushinda tuzo ainati.

"Nilipigwa 2k manze na CMOs, kwanza nilishtuka manze juu kuangalia hii song yangu ndio imepiga number one kila mahali, imeshinda Groove Awards, halafu ukiangalia wame wamekuwa ranked kwamba huyu ndio amekula the highest, ilinipiga shock," Jabidii alisema.

Kutokana na ukweli huo machoni pake, Jabidii alisema alihisi kabisa muziki ni utapeli na hata akawaza kuachana nao.

"Kwanza ilinipiga shock ikanihit manze muziki is a scam. Lakini with time timetoa hizo ngoma zingine, Vimbada, Makofi....so hatuwezi ngoja kuna ngoma ingine itakuja kubadilisha life. So all this time nimelearn kusurvive bila sijui nangoja royalty kutoka wapi na wapi," aliongeza.

Kwa sasa msanii huyo wa hit song ya Makofi anazidi kitamba ya kibao cha 'Miel Matin' ambacho ameshirikiana na mamake, Ayun Nyapolo na kuwavutia wengi haswa kwenye jukwaa la TikTok. 

View Comments