In Summary

• Mama huyo wa watoto wawili alisema kwamba kinachozua mvutano na mkwamo aghalabu kwenye ndoa ni wanandoa kuwa na kiburi.

Size 8.
Image: Screenshot

Mchungaji na mwinjilisti Size 8 amevunja kimya chake kuhusu suala la ndoa siku chache baada ya kudai kuachana na mpenzi wake Dj Mo.

Akizingumza kwenye Obinna Show Live, Size 8 alikiri kwamba kila ndoa ina changamoto zake lakini akasema kwamba watu wengi katika ndoa huwa wanajitakia changamoto hizo wenyewe.

Mama huyo wa watoto wawili alisema kwamba kinachozua mvutano na mkwamo aghalabu kwenye ndoa ni wanandoa kuwa na kiburi.

"Kila ndoa ina pandashuka zake. Ambacho ningependa kuwashauri wanawake ni kwamba siri moja kwa ndoa bila shaka ni Yesu Kristo, kumweka Mungu katikati na unyenyekevu," Size 8 alisema.

"Shida ya watu wengi kwa ndoa ni kiburi, nyinyi wote mkipanda na kiburi, nani atashikilia ndoa? Hivyo silaha kubwa kwa ndoa ni unyenyekevu, hata kwa wanaume pia," aliongeza.

Mchungaji huyo aliwasuta wanaume ambao wana dhana kwamba unyenyekevu na kusalimiaha ni majukumu ya mwanamke tu katika ndoa.

Alisema kwamba kigezo cha kwanza ambacho kinastahili kuonekana kutoka kwa washirika wote katika ndoa ni unyenyekevu.

"Wanaume, kigezo kimoja cha mapenzi ni unyenyekevu. Wanaume wengi hawana hilo. Wanaume wengi hawana unyenyekevu wa kumkubalia hata mke wake kufanya anachopenda kufanya."

"Na wanawake hawana unyenyekevu wa kujisalimisha kwa wanaume wao. Mwanaume, mkubalie mkeo kuwa jinsi atakavyo na wewe mke, jisalimishe kwa mamlaka ya mumeo," alishauri.

View Comments