logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Background ya mtu huamua 80% ya jinsi atakavyokuwa katika ndoa - Size 8

So huwezi sema, 'yeye mbona hana tabia kama yangu'...aje na hakulelewa hivyo? - Size 8.

image
na Davis Ojiambo

Burudani09 August 2024 - 07:49

Muhtasari


  • • Size 8 alifichua kwamba mpenzi wake DJ Mo alilelewa na mzazi mmoja na ilimchukua muda kuja kuingiana naye.
  • • Msanii huyo wa injili alisema kwamba mtu ambaye amelelewa na mzazi mmoja ni tofauti sana na mtu ambaye amelelewa na wazazi wote.

Pasta Size 8 ameeleza kwa nini ni vizuri mtu kupata ufahamu wa kina kuhusu usuli wa mpenzi wako kabla ya kuingia katika ndoa.

Size 8 anahisi kwamba usuli na mazingira anakolelewa mtu utotoni huamua pakubwa tabia zake baadae maishani.

Msanii huyo wa injili alisema kwamba mtu ambaye amelelewa na mzazi mmoja ni tofauti sana na mtu ambaye amelelewa na wazazi wote.

Size 8 anawarai wachumba kuwaelewa wenzao kutokana na mazingira ya makuzi yao utotoni ili kurahisisha uhusiano katika ndoa.

"Kuna kitu kimoja ambacho watu huwa hawaangalii katika ndoa. Watu hutoka katika usuli tofauti. Mimi nimelelewa kutoka kwa mazingira tofauti na DJ Mo. Tabia ya mtu aliyelelewa na mzazi mmoja haiwezi kuwa sawa na ya yule amelelewa na wazazi wote," alisema.

"Katika ndoa, jaribu kuelewa ni wapi mpenzi wako alikotokea. Kwa sababu usuli wake unaamua 80% ya yeye ni nani. Na huwezi badilika kwa usiku mmija tu, unalipa muda," aliongeza.

Size 8 alifichua kwamba mpenzi wake DJ Mo alilelewa na mzazi mmoja na ilimchukua muda kuja kuingiana naye.

"Kama Mo alitoka katika mazingira ya kulelewa na mzazi mmoja kwa muda mrefu alikuwa anaona vitu vingi mamake akifanya. Vitu ambavyo mimi nilijua ni majukumu ya baba, Mo aliyajua kuwa ya mama," Size 8 alifunguka.

"So wezi sema, 'yeye mbona hana tabia kama yangu'...aje na hakulelewa hivyo? Hajazoea. Unaina hiyo kuzoea na kupatiana muda wa kukua ni muhimu. Ndio maana najivunia mume wangu kwa sababu yeye ni baba ambaye hakuwahi muona," aliongeza kwa hisia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved