Mchungaji wa kanisa moja nchini Nigeria amegonga vichwa vya habari baada ya taarifa kuhusu mapato anayojizolea kutoka YouTube kuenezwa.
Kwa mujibu wa taarifa, mchungaji Jerry Uchechukwu Eze wa kanisa la Joy International ndiye anayeongoza nchini humo kwa watu wanaolipwa hela ndefu na jukwaa la YouTube.
Pasta Eze anasemekana kuwekeza katika video nzuri jambo ambalo linavutia wengi kwa video za mafunzo yake kwenye jukwaa hilo.
Playboard, jukwaa la kuonyesha deta za malipo ya YouTube ilidhihirisha kwamba pasta huyo anatengeneza zaidi ya Naira milioni 7 kila siku kutoka YouTube, kiasi sawa na Ksh 565, 840.
Deta hiyo ilionyesha kwamba mchungaji huyo ndiye anashikilia nafasi ya kwanza kwa wanaolipwa na YouTube nchini humo kwa kupokezwa kiasi cha Naira bilioni 7, sawa na shilingi milioni 564.745 pesa za Kenya.
Deta zilionyesha kwamba mnamo Julai 16, 2023, alipata mapato ya ajabu ya N21 milioni, sawa na shilingi za Kenya 1.7M kwa siku moja kutokana na kuongezeka kwa trafiki ya wageni kwenye ufuatiliaji wa video zake YouTube.
Chaneli ya kanisa lake ina wafuasi 2.1M wanaofuatilia na maidhui yake aghalabu huwa kutiririsha mikutano ya ibada na maombi.
Juhudi kubwa za mchungaji zinajumuisha takriban video 1,500 kila wiki, kufanya hadhira yake kushughulikiwa na kituo chake kustawi.