Mwanasosholati Huddah Monroe amefunguka kwamba anahitaji angalau dola elfu 70, sawa na shilingi milioni 9 pesa za Kenya kila mwezi ili kuishi kwa raha mstarehe bila matatizo yoyote ya kifedha.
Huddah aliweka fikira zake wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alikuwa akitoa maoni kwa moja ya utafiti uliofanywa kubaini kiasi cha pesa ambacho mtu wa kawaida anahitaji kila mwezi ili kuishi kwa raha bila matatizo.
Katika utafiti huo wa St Petersburg huko Urusi ambao alichapisha picha yake kwenye skrini, mtu mzima ambaye hana familia anahitaji shilingi milioni 12 kwa mwaka ili kuishi kwa raha mstarehe huku watu wawili wazima wanaofanya kazi pamoja na wanao wakiwa wanahitaji shilingi milioni 27 kwa mwaka.
Kwa upande wake, Huddah alisema yeye kwa vile ni mtu mzima bila watoto, angehitaji angalau shilingi milioni 9 kwa mwezi ili kuishi maisha yasiyojua taabu na shida za kifedha.
“Nahitaji angalau $70,000 – sawa na Sh9m na kwa kawaida inawezekana. Mungu ndiye mkubwa,” alisema huku akiambatanisha chapisho hilo na wimbo wa Vybz Kartel, Without Money.
Mrembo huyo alizidi kusema kwamba kila mara anapoumbuka kuhusu safari yake ya maisha kuelekea utajiri wake, anakumbushwa na nyimbo nyingi za msanii Vybz Kartel ambaye amekuwa akimsifia tangu mwishoni mwa wiki jana.