In Summary

• Taarifa za kifo cha Mandojo zilithibitishwa na msanii mwenzake, Soggy Doggy, ambaye alionyesha masikitiko yake makubwa kwenye mitandao ya kijamii.

MADONJO.
Image: HISANI

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Madonjo, maarufu kutoka kwa kundi la Madonjo & Domokaya amefariki baada ya kushambuliwa na halaiki.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Madonjoo aliuawa siku chache kuelekea siku yake ya kuzaliwa na umati uliomdhania kimakosa kuwa ni mwizi jijini Dodoma.

Mwanamuziki huyo maarufu kwa nyimbo zake za "Nikupe" na "Dingi," alipigwa kikatili hadi kufa katika tukio ambalo limewashangaza mashabiki na wafuasi wake.

Taarifa za kifo cha Mandojo zilithibitishwa na msanii mwenzake, Soggy Doggy, ambaye alionyesha masikitiko yake makubwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Moyo wangu una maumivu makali; Nitakukumbuka sana kaka na rafiki yangu. Pumzika kwa amani Mandojo. Hakika maisha ya mwanadamu ni mafupi sana hapa duniani. Pole kwa ndugu, jamaa, na marafiki, na pole sana kaka yangu @domokayatz. Kazi ya Mungu haina makosa,” Soggy Doggy aliandika.

Risala pia zilimiminika kutoka kwa Domo Kaya, rafiki wa karibu na mfanyakazi mwenza wa Mandojo. Katika chapisho la moyoni, Kaya aliomboleza wakati wa mkasa huo.

“Daaaah MWANANGU, siamini tarehe 22 mwezi huu inatakiwa iwe siku yako ya kuzaliwa. Aisee, kwanini! Hii inasikitisha sana. Pumzika kwa amani, Mungu akupe mwanga wa milele rafiki, kaka,” Domo Kaya aliandika.

Kifo cha Mandojo kinakuja siku chache kabla ya siku ya kuzaliwa kwake Agosti 22.

Wawili hao walivuma na vibao vingi kuanzia mwaka wa 2004 kama vile Nikupe Nini, Wanoknok, Niaje, Nizikwe Hai, Taswira, Nihukumu Mola, Fani Yangu, Ni Rafiki Tu miongoni mwa ngoma zingine.

View Comments