logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Sijazeeka, ni ugonjwa wa moyo ninaougua unaonifanya kuonekana mzee” - Nyako (video)

Itakumbukwa hii si mara ya kwanza kwa Nyako kuzungumzia hali ya tatizo lake la ugonjwa wa moyo.

image
na Davis Ojiambo

Burudani13 August 2024 - 11:33

Muhtasari


  • • Itakumbukwa hii si mara ya kwanza kwa Nyako kuzungumzia hali ya tatizo lake la ugonjwa wa moyo.
  • • Miezi mitatu iliyopita katika video kwenye TikTok yake, Nyako alijitabiria kifo akisema kuwa hadhani ataishi zaidi ya miaka 3 ijayo.
NYAKO

TikToker Nyako Pilot kwa mara nyingine amewajibu wale wanaomkejeli muonekano wake wakidai kwamba umri wake umeenda na kwamba amezeeka.

Katika video ya hivi karibuni kwenye TikTok, Nyako alifafanua chanzo cha muonekano wake kuwa wa uzee, akisisitiza kwamba yeye bado ni kijana ila tatizo la ugonjwa wa moyo ndilo linamfanya kuonekana mzee.

“Mimi sijazeeka, niko na tatizo la moyo ambalo linanifanya kuonekana mzee kuliko umri wangu. Mimi si mzee,” alisisitiza.

TikToker huyo anayeishi nchini Ujerumani alitoa mfano wa maisha jinsi yamekuwa mafupi akistaajabu jinsi bintiye mwigizaji Nyaboke alivyofariki.

“Maisha siku hizi ni mafupi, angalia Marrie, amekufa na umri wa miaka 19. Nani anataka wanawe kufa wakiwa wadogo hivyo? Nani? Nyinyi watu, kama bado unaishi shukuru, ni Baraka na pia kuishi ni bahati. Siku hizi ukifika 40 shukuru Mungu,” Nyako alishauri.

Itakumbukwa hii si mara ya kwanza kwa Nyako kuzungumzia hali ya tatizo lake la ugonjwa wa moyo.

Miezi mitatu iliyopita katika video kwenye TikTok yake, Nyako alijitabiria kifo akisema kuwa hadhani ataishi zaidi ya miaka 3 ijayo.

“Kama sitakuwa nimekufa katika kipindi cha miaka 3 ijayo, nitakuwa muujiza unaoishi. Lakini mwisho wa kwisha, sisi wote kwa wakati Fulani tutakufa, uwe mgonjwa usiwe mgonjwa, kifo lazima kitatembelea kila mtu. Mimi kile ninawaomba kuwa makini sana jinsi unavyowafanyia watu, usiwaumize watu,” Nyako alishauri baina ya sauti nzito yenye huzuni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved