Kupitia mtandao wake wa facebook na Tiktok msanii Stevo Simpleboy a.k.a "King of Africa " kama anavojiita aeleza kwamba msanii wa bongo Diamond Platnumz alimtexti instagram akitaka collabo.
Aidha Simple Boy amesema kua uamuzi huo unakuja baada ya Diamond kukataa kufanya colabo na wasanii wa Kenya .
"Shega" moja yake ya vibao vya simpleboy ambavyo vinazidi kufanya vizuri umu huku kikiwa kinakubalika na wasanii wenza kwa kipindi cha wiki mbili zilizo pita .Vilevile Stevo amemwomba Diamond ikiwa hataweza kuafikia zile hela ni bora aachane na mambo ya colabo.
Aidha ,Stevo Simpleboy amekua katika akili za wakenya kupitia mavazi yake ambayo yanaupekee akisema kua yeye yuko vizuri na mitindo yake ni ya upekee hasa ya mavazi.
Vilevile msanii Simpleboy ameonyesha umahiri wake hasa kwa mtandao wa Tiktok akiwa msanii mwenye ufuasi mkubwa kwenye mtandao huo kwa video zake ucheshi na misamiati ambayo imekua ikitumika miongoni mwa video za ucheshi kwenye sanaa hiyo.