Mshindi wa tuzo ya Afrimma kitengo cha msanii bora wa kike Afrika mashariki, Nadia Mukami atakuwa na jambo kubwa mwishoni mwa mwezi Agosti.
Kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, Mukami alitangaza kwamba maandalizi yote yamekamilika kuelekea siku yake kuu, Agosti 30 ambapo anatarajia kuzindua albamu yake nyingine.
Mama huyo wa mtoto mmoja alifichua kwamba albamu yake itakwenda kwa jina ‘Queen of the East’ na ambayo itakuwa albamu yake mzima ya kwanza tangu ajitose kwenye Sanaa ya muziki mapema mwaka 2018.
“Ninawatambulishia album yangu ya kwanza, malkia wa mashariki tarehe 30 agosti 2024!!!Hifadhi kupitia link kwenye bio,” aliandika.
Mukami hakuweka wazi albamu hiyo itakuwa na ngoma ngapi kwa jumla.
Hata hivyo, itakumbukwa hii si mara ya kwanza anatoa mkusanyiko wa ngoma nyingi kama nusu albamu maarufu EP.
Tanfu aingie kwenye Sanaa, ametoa EP tatu ambazo zote zimefanya vizuri na sasa anatarajia kujitupa mazima kwenye uzinduzi wa albamu mzima kwa mara ya kwanza.
Alianza na EP ya African Popstar ambayo aliiachia Septemba 2020 kisha 2022 akaachia EP nyingine kwa jina Bundle of Joy na mwaka jana alishirikiana na mumewe Arrow Bwoy wakatoa EP kwa jina Love & Vbes.