Mfanyibiashara Shakib Lutaaya Cham ameshauriwa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mke wake, Zari Hassan, kufuatia mzozo unaoendelea katika uhusiano wao.
Jackson Mucunguzi, afisa mkuu wa polisi nchini Uganda, hivi majuzi alienda kwa X kumshauri kijana huyo kumfungulia Zari kesi kwa kile alisema kwamba mjasiriamali huyo mama wa watoto watano anamtumia vibaya kijana wa watu.
Mucunguzi alimshauri Shakib kwamba ikiwa anajua haki zake, anaweza kupiga hatua na kumfungilia Zari kesi ya ukatili wa nyumbani wa kiuchumi na kisaikolojia, baada ya mwanamama huyo kudai kwamba Shakib hakuwa anachangia chochote kiuchumi katika ndoa yao.
“Iwapo ndugu yangu Shakib akiwa mtu mzima atakusanya imani na kujua haki zake👮, kesi ya unyanyasaji wa kiuchumi na kisaikolojia wa nyumbani; inaweza kusajiliwa katika @PolisiUg, Idara ya Ulinzi wa Mtoto na Familia na kusikilizwa kwa mafanikio katika mfumo wa Haki wa Uganda,” Afisa huyo wa polisi aliandika, akisisitiza ni wakati maisha ya mtoto wa kiume pia yasingatiwe kuwa na umuhimu.
Mvutano kati ya Shakib na Zari uliongezeka baada ya Zari kumkaribisha aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz, nyumbani kwake nchini Afrika Kusini kusherehekea siku ya kuzaliwa ya binti yao Latifah Dangote.
Katika ujumbe wake wa sauti, Lutaya, ambaye pia anajulikana kama Cham, alieleza kuwa vitendo hivyo vimemletea aibu mara kwa mara na kuathiri vibaya afya yake ya akili.
Akijibu, Zari ambaye alionekana kulewa na baadhi ya watazamaji alidai kuwa hakumualika Platnumz Afrika Kusini.
Pia alimkumbusha Shakib kwamba mwimbaji huyo wa Tanzania si tishio tena, akisema walikuwa wameshashibana miaka mingi iliyopita.
Zaidi ya hayo, alimwambia mume wake waziwazi kwamba hawezi kuweka sheria katika uhusiano wao kwani michango yake ni ndogo.