Mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za Afro kutoka Nigeria Tiwa Savage amewaacha baadhi ya mashabiki wake na maswali baada ya kudokeza kuwa yeye hupenda kuwa kwenye mahusiano na wanaume wenye umri zaidi ya 50 na ambao wako tayari kutumia hela kwake. .
"Sipendi kuingia kwenye uhusiano na wavulana au wanaume wa umri wa miaka 30 hadi 40 ,kwasababu wanachokitaka ni ngono tu."
Aidha aliongeza kusema kuwa,"Type yangu ni wanaume wa angalau miaka 50 na kuendelea ambao wako tayari kutumia pesa nyingi sana kwangu."
Ni gumzo ambalo linazidi kuonekana mitandaoni baada ya kuwa ana ufuasi mkubwa kutoka kwa wanaume wa umri mdogo kutokana na urembo wake wenye mvuto asilia ,na ngoma zake kukubalika kote Afrika na pia nje ya Afrika na kupata ufuasi mkubwa kutokana na utunzi wake usio linganishwa.
Savage amekuwa msanii ambaye amekua akijituma katika fani hiyo na kushinda mataji mbali mbali kama vile Soundcity MVP Awards mwaka wa 2020 na vile vile MTV Europe Music Awards mwaka wa 2018 na kuonyesha umahiri wake na bado kuendelea kufanya vizuri na kuchaguliwa katika tuzo mbali mbali .