logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Rue Baby amefanya mpaka sasa sijapata mke wa kuoa” – MCA Tricky

Msanii huyo alisema kuwa warembo wengi wanaogopa mamake Rue Baby, Akothee wakisema vile ni mtu wa drama.

image
na Davis Ojiambo

Burudani21 August 2024 - 10:04

Muhtasari


  • • Msanii huyo alisema kuwa warembo wengi wanaogopa mamake Rue Baby, Akothee wakisema vile ni mtu wa drama.
TRICKY NA RUE

Mchekeshaji MCA Tricky amefunguka athari ambazo ukaribu wake na bintiye msanii Akothee, Rue Baby zimeleta katika maisha yake ya kimapenzi.

Akizungumza na Obinna, Tricky alifichua kwamba ukaribu wake na Rue Baby uliwafanya wengi kuamini kwamba wawili hao walikuwa wanachumbiana, kiasi kwamba mpaka sasa hawezi tongoza mrembo yeyote bila kuulizwa swali la hali ya ‘uchumba’ wake na binti huyo wa Akothee.

“Rue Baby amenifanya nisipate mke, siwezi mtongoza mrembo yeyote akose kuniambia stori za Rue. Siku hizi hata najaribu kutongoza mrembo ananiambia atakubali kwa sharti kwamba Rue Baby asijue,” Tricky alisema.

Msanii huyo alisema kuwa warembo wengi wanaogopa mamake Rue Baby, Akothee wakisema vile ni mtu wa drama.

Cha kushangaza, Tricky alisema kwamba hata Rue Baby naye amekuwa akimuambia kwamba ukaribu wake na yeye umemponza katika maisha yake ya kimapenzi kwani hawezi kupata mpenzi.

“Hata yeye ananiambia hivyo kwamba mwanamume akimtongoza anaambiwa nisijue, uhusiano wangu na Rue Baby haukuwa uhusiano wa kimapenzi,” Tricky aliongeza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved