Difella Music, Mkenya anayetamba kuwa anamfanana gwiji wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefichua kwamba amepunguza unywaji wa pombe.
Kupitia video walipokuwa wakihojiwa Diamo nd feki alieleza kuwa amebadilisha maisha ambayo alikwa akiishi baada ya kuwa na umaarufu.
"Nimepunguza pombe juu kutoka nikuwe famous,nikiingia mahali labda nikunywe 20k juu ya kununulia watu", alisema.
Aidha, Remcy Don almaarufu Kenyan Derulo ameeleza kuwa aliongea na Jason Derulo na akamwambia kuwa ule wakati atakuwa akija Dubai ndipo wataonana.
Aidha kenyan Diamond amesema kuwa yeye ni mchapakazi katika tasnia ya muziki na angependa Diamond Platinumz kumtambua katika kazi yake anayohifanya.
Vile vile, wamesema kuwa wako na kitu kipya ambacho wanazidi kukipika pamoja na wanaamini kuwa watu watakipenda kutokana na wao kuwa na talanta .
Kenyan Diamond ,amesema kuwa yeye alianza usanii kutoka kitambo licha ya wakenya kumjua baada ya video waliofanya na Remcy Don.
Aidha Remcy amesema hapo awali akuwa na hela za kutolesha video lakini kwa sasa yuko vizuri na kwasasa ametolesha ngoma yake iliyokosti 600k pesa za Kenya.
Remcy ameelezea kuwa alipitia changamoto ili kumfikia Jason Derulo lakini sasa wanajuana na Remcy yuko tayari wafanywe collabo.