logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Willy Paul akiri upendo mkubwa kwa baby mama wake mzungu na binti yao

"Nawapenda hawa binadamu wawili," alisema

image
na Radio Jambo

Habari17 February 2023 - 08:12

Muhtasari


•Willy Paul alichapisha picha nzuri za mzazi mwenzake Viktoriya Shcheglova pamoja na mtoto wao Sonya Wilsovna na kueleza jinsi anavyowapenda.

•Mwimbaji huyo alijivunia maendeleo ya binti huyo wake wa miaka minne na kufurahia jinsi alivyokua kuwa mkubwa.

Mwanamuziki wa nyimbo za mapenzi Wilson Radido almaarufu Willy Paul ameonyesha upendo mkubwa kwa familia yake ya Kirusi.

Siku ya Ijumaa asubuhi, mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili alichapisha picha nzuri za mzazi mwenzake mzungu, Viktoriya Shcheglova pamoja na mtoto wao Sonya Wilsovna na kueleza jinsi anavyowapenda.

Willy Paul alijivunia maendeleo ya binti huyo wake wa miaka minne na kufurahia jinsi alivyokua kuwa mkubwa.

"Mtazame binti yangu Sonya, amekuwa mkubwa! Muda haungojei mtu walahi. Nawapenda hawa binadamu wawili," alisema chini ya picha hizo.

Mwanamuziki huyo aliyezingirwa na utata mwingi kwenye taaluma yake ya takriban mwongo mmoja alihoji ni nini alichofanya ili kustahili familia nzuri kama hiyo. Pia aliahidi kuendelea kuachia muziki zaidi.

Mwaka wa 2021, Willy Paul alibainisha upendo wake mkubwa kwa familia hiyo yake na kuahidi kumshughulikia bintiye kwa hali na mali.

"Binti yangu Sonya na mama yake wanatulia tu. Kama baba, nitafanya kila kitu kumlinda binti yangu" Willy Paul aliandika video ya Mama Sonya akiwa amemshika binti huyo wao huku wakisikiliza wimbo wake 'My Woman.

Mwimbaji huyo alitangaza kuzaliwa kwa binti yake, Sonya na mwanamitindo huyo wa Kirusi mwishoni mwa mwaka 2020.

Sonya ni mtoto wa pili wa  Willy Paul ambaye anajulikana.

Mwanamuziki huyo ambaye kwa kawaida huficha mahusiano yake ana mtoto mwingine, King Damian Radido Opondo ambaye alipata na mwanadada wa hapa nchini anayemtambulisha tu kama Mama Damian.

Hata hivyo, mara nyingi ameonekana kumpendelea zaidi baby mama wake Mrusi na inaaminika huenda bado wako kwenye mahusiano ya mbali. Willy alimshirikisha Mama Sonya katika video ya kibao chake 'My Woman' .


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved