In Summary

•Mwanadada mmoja alihapisha ujumbe kwenye mtandao wa Twitter akisema kwamba mama yake mwenye umri wa miaka 60 anahitaji mwanamume.

•Baadhi ya wanamitandao walipendekeza mamake ajihusishe na kazi zingine mbadala ili zimtolee upweke huo.

Ndoa
Image: star

Mwanadada mmoja wa makamo alizua gumzo mitandao ya kijamii baada yake kuchapisha ujumbe kwenye mtandao wa Twitter akisema kwamba mama yake mwenye umri wa miaka 60 anahitaji mwanamume.

Katika chapisho hilo, mwanadada huyo alieleza kwamba mama yake hana mume na ni mpweke sana huku akiwaomba wanaume wanaotaka mke wajitokeze.

Kulingana na mwanadada huyo, mwanawake hapaswi kuwa na huzuni au kuzeeka bila kuolewa huku akisema sio jambo nzuri kutokuwa na mwenzi.

''Mama yangu mmoja mwenye umri wa miaka 60 na zaidi anahitaji mwanaume. Yeye ni mpweke sana. Hii ndio sababu nasema manawake sio sawa wanawake kuzeeka bila ndoa na kuwa wapweke. Usizeeke peke yako.'' alisema.

Wanamitandao walionyesha kuchangamka na kutuma misururu ya jumbe huku wengi wakimtakia mema mwanamke huyo apate mwenzi.

Jo Cretor alisema ''Najua maombi hufanya kazi. Aombe na ata atapewa mahitaji yake''

Jeena WL alisema ''Ningependekeza atafute njia ingine ya kutimiza upweke. Kunao wanawake wengi hawana bwana ila maisha yao ni ya furaha.''

Nakia alisema ''Mama yangu anahitaji kuchumbiana pia. anafaa aanze kuacha kudate wanaume pia kwa sababu kuna wengine pia hawana''

NewNamels aitoa ushauri na kusema, ''Ingekuwa bora zaidi kama ungetafutia mamayako kazi mbadala ya kufanya kama vile biashara ama ajihusishe na shughuli anazozipenda na atakuwa na furaha sana ikilinganishwa na akiolewa''

View Comments