In Summary

•Otile Brown alifichua kwamba yeye na mpenzi wake walitarajia mtoto wa kiume, hata hivyo mtoto huyo hakufanikiwa

•Mtunzi huyo wa kibao cha ‘Nabayet’ alikiri kwamba kupoteza ambaye angekuwa mtoto wake wa kwanza kulimbadilisha sana.

Image: INSTAGRAM// OTILE BROWN

Mwimbaji wa Kenya Jacob Obunga almaarufu Otile Brown amedokeza kwamba hajakuwa akiendelea vizuri tangu alipompoteza mtoto wake ambaye bado hakuwa amejazaliwa.

Katika taarifa yake siku ya Jumapili, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 30 alifichua kwamba yeye na mpenzi wake walitarajia mtoto wa kiume, hata hivyo mtoto huyo hakufanikiwa.

"Alikuwa mvulana. Dah.. Yote ni sawa. Angekuwa besti wangu,” Otile Brown aliandika kwenye Instagram.

Brown alifunguka kuhusu jinsi yule ambaye angekuwa mzazi mwenzake alihusisha kifo cha mtoto wao na hisia mbaya kwenye mitandao ya kijamii baada ya yeye kufichua kuwa alikuwa anatarajia mtoto wake wa kwanza mapema mwezi uliopita, hatua ambayo sasa anajutia.

“Mwanzoni nilichukia mitandao ya kijamii kwa sababu alinichukia na kunifanya niamini kuwa hiyo ni hisia mbaya kwenye mitandao ya kijamii na ni kama ninaamini kwa sababu kwa mtu ambaye hajawahi kutangaza maisha yake kwenye mitandao ya kijamii, kwa bahati mbaya niliamua kuchapisha kuhusu hilo huku moyo wangu ukiniambia nisifanye hivyo, ilinifanya nijihisi kuwa na hatia,” alisema.

Aliongeza, "Lakini tena nilisema siwezi kuipa misismko hii ya chini nguvu nyingi. Huenda ni kosa letu, mpango wa Mungu au sababu za kawaida. Huwezi kubishana nami, haki ya Mungu.”

Mtunzi huyo wa kibao cha ‘Nabayet’ alikiri kwamba kupoteza ambaye angekuwa mtoto wake wa kwanza kulimbadilisha sana.

“Nimekuwa nikihisi huzuni. Nimekuwa nje ya nchi nikiharibu kadi yangu ya malipo, nikijiadhibu. Huwa ninaomboleza tofauti,” alisema.

Mwanamuziki Otile Brown alitangaza kifo cha mtoto wake ambaye bado hakuwa amezaliwa mapema mwezi huu.

Katika taarifa yake, mwimbaji huyo alifichua kwamba yule ambaye angekuwa mtoto wake wa kwanza hakufanikiwa.

"Mtoto wetu hakufanikiwa.. Nadhani sio mwaka wangu pendwa tena," Otile Brown alisema kwenye mtandao wa Instagram.

Aliongeza, "Yote ni nzuri. Mungu unajua sijawahi kukuuliza wala kukuhoji.. ninachofanya ni kutabasamu na kuwa sawa.

Haya yalijiri takriban wiki moja tu baada ya mwanamuziki huyo mzaliwa wa Pwani kutangaza anatarajia mtoto wake wa kwanza.

Katika taarifa yake mwezi uliopita, mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 30 aliapa angempa mtoto wake upendo wake wote.

"Bizeee hivi karibuni atakuwa papa, Inshallah.. Nitakupenda sana mtoto #Inshaallah," Otile Brown alisema kupitia mtandao wa Instagram.

Brown hata hivyo hakufichua maelezo ya mwanamke ambaye angekuwa mzazi mwenzake au jinsia ya mtoto aliyetarajia.

View Comments