In Summary

•Habari za kifo cha mke wa Makokha, Bi Purity Wambui zilitangazwa na muigizaji Ondiek Nyuka Kwota mnamo Jumapili jioni.

•Ondiek aliwaomba mashabiki waiweke familia ya Makokha katika maombi na kuendelea kuwapa sapoti wakati huu mgumu.

Muigizaji Alphonse Makhoha amefiwa na mke wake Purity Wambui.
Image: FACEBOOK// ONDIEK NYUK KAKWOTA

Wakenya wameungana na familia na marafiki wa mwigizaji na mchekeshaji mkongwe Matayo Keya almaarufu Alphonse Makokha Makacha kufuatia kifo cha mke wake mpendwa

Habari za kifo cha mke wa Makokha, Bi Purity Wambui zilitangazwa na muigizaji mwenzake katika kipindi cha Vioja Mahakamani Ondiek Nyuka Kwota mnamo Jumapili jioni.

Katika tangazo alilotoa kwenye mtandao wa Facebook, Ondiek alimuomboleza marehemu Wambui kama mwanamke wa kipekee aliyegusa maisha ya wengi.

"Wapendwa marafiki na mashabiki, Ni kwa huzuni kubwa kwamba tunashiriki habari za kuhuzunisha za kutoweka kwa Purity Wambui, mke mpendwa wa Makacha Aka "Babyface" Wa Vioja Mahakamani Kwenye KBC Channel 1 TV," Ondiek alitangaza kupitia akaunti yake ya mtandao wa Facebook.

Aliongeza, "Alikuwa mwanamke wa ajabu ambaye aligusa maisha ya watu wengi kwa wema wake na uchangamfu. Matayo Keya almaarufu Makokha Makacha Na familia yake wanashukuru sana kwa upendo na msaada wenu katika Msimu huu mgumu sana."

Ondiek aliwaomba mashabiki waiweke familia ya Makokha katika maombi na kuendelea kuwapa sapoti wakati huu mgumu.       

"Kwa wale wanaotaka kutoa rambirambi zao, tafadhali jisikie huru kuacha jumbe zako hapa chini. Mawazo na maombi yako yanathaminiwa sana. Asante kwa uelewa wako na msaada," alisema.

Hakuna mengi yanayojulikana hadharani kuhusu marehemu Purity Wambui kwani ni nadra sana kwa muigizaji Alphonse Makokha kuonyesha familia yake hadharani.

View Comments