In Summary

• Seneta Karen Nyamu ameweka wazi  kuwa baba wa watoto wake wawili wadogo, Samidoh ni milionea.

•Wapenzi hao walimpokea mtoto wao wa pili, msichana mwaka jana na penzi lao limeonekana kuendelea kunoga kila uchao.

Samidoh na Karen Nyamu
Image: HISANI

Seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu ameweka wazi kuwa mzazi mwenzake, mwimbaji Samuel Muchoki almaarufu Samidoh si mtu maskini.

Wakati akijibizana na wafuasi wake kwenye mtandao wa Facebook, Nyamu alifichua kuwa baba huyo wa watoto wake wawili wadogo ni milionea.

Shabiki mmoja alikuwa ametoa maoni chini ya moja ya machapisho yake akimtaka amsaidie mpenzi wake Samidoh kupata kitu kutoka kwake akibainisha kuwa seneta huyo haishi na mwimbaji Mugithi licha ya kuwa wanachumbiana.

“Msaidie Samidoh pia atoke kwako akiwa na kakitu. Uliolewa na hukai kwa mwanaume,” mtumiaji wa Facebook aliandika kwenye ukurasa wake.

Karen Nyamu alijibu, "Yule ni millionare mama we don’t date broke men sorry."

Kumaanisha: “Yule ni millionea mama hatuchumbiani na wanaume fukara.”

Katika chapisho hilo, seneta huyo wa kuteuliwa wa UDA alithibitisha kwamba ni maombi yake kwamba mke wa Samidoh, Bi Edday Nderitu siku moja atarudiana na mwimbaji huyo ili wawe familia moja kubwa.

Shabiki mmoja aliandika, "Siku moja familia ya Edday itaungana tena."

Bila kusita, seneta Nyamu alionekana kukubaliana na maoni ya shabiki huyo na wakati huo akadokeza kwamba angefurahi sana kuona familia ya Muchoki ikiungana na kuwa kubwa tena.

“Ni maombi yetu pia. Tukue familia moja kubwa.”

Katika maoni mengine, shabiki alimuuliza jinsi alivyokuwa akimsaidia mke huyo wa Samidoh kujibu maombi yake.

‘Nashangaa ni maombi gani ya (Edday) ambayo Mungu anajibu kupitia wewe,” Mtumiaji wa Facebook aliuliza.

Karen alijibu, “Mungu atatumia watu wengine kuniamini.

Seneta Nyamu amekuwa akitumia wakati mzuri na mzazi mwenzake, Samidoh katika wiki za hivi majuzi wakati mke wa mwimbaji huyo wa Mugithi akiaminika kuwa Marekani ambapo anafurahiya muda na watoto wake na marafiki wengine.

Mahusiano ya wawili hao yaliibuka hadharani mwaka wa 2021 kufuatia kuzaliwa kwa mwana wao, Sam Junior mwaka wa 2020.Wawili hao walikuwa wakichumbiana nyuma ya pazia kwa muda kabla ya mapenzi yao hatimaye kujulikana hadharani.

Wapenzi hao walimpokea mtoto wao wa pili, msichana mwaka jana na penzi lao limeonekana kuendelea kunoga kila uchao.

View Comments