In Summary

•Akothee alimshukuru mpenzi huyo wake wa zamani kwa kumsaidia kujenga jina lake na kumlinda alipokabiliwa na matatizo.

•"Unathaminiwa, unatambuliwa, unaheshimiwa na unapendwa, tembea na kichwa chako juu, kwa sababu wewe ni fahari ya Kamagambo,” Akothee alimwambia Nelly Oaks.

Nelly Oaks na Akothee
Image: INSTAGRAM//NELLY OAKS

Siku ya Ijumaa, mwanamuziki na mfanyabiashara mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee alimsherehekea mpenzi wake wa zamani na meneja wake Hezekiah Nelson Oyugi almaarufu Nelly Oaks kwa njia maalum wakati akiadhimishaa siku yake ya kuzaliwa.

Katika taarifa ndefu kwenye mtandao wa Facebook, mama huyo wa watoto watano alimmwagia sifa Nelly Oaks kwa jukumu kubwa ambalo amecheza katika maisha yake na biashara yake ya sanaa.

Akothee alimshukuru mpenzi huyo wake wa zamani kwa kumsaidia kujenga jina lake na kumlinda alipokabiliwa na matatizo.

“Asante sana kwa sehemu uliyocheza katika maisha yangu yote na kazi yangu, ni sisi wawili tu tunaojua jinsi tulivyoipata brabd hapo ilipo. Asante sana kwa kuwepo wakati ulimwengu ulionekana kama damu ndani ya giza. Asante kwa kunifuta machozi, kusimama pamoja nami wakati baba wa watoto walipokusanyika dhidi yangu huko Uswizi, hiyo ilikuwa MBAYA. Unasimama nami,” Akothee alimwandikia Nelly Oaks kupitia ukurasa wake wa Facebook siku ya Ijumaa.

Aliongeza, "Unakumbuka bilione akiniambia niache muziki, nifute chaneli yangu ya YouTube, nifute akaunti zangu za mitandao ya kijamii na nibaki nyumbani?? Ulisimama kidete kumshawishi kuwa brand soon itajitengenezea pesa zake sio kupoteza muda wala kupoteza pesa, Tena asante kwa kuniamini. Ulinilinda mimi na brand kama tulikuwa mapacha.”

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 alimhakikishia Nelly Oaks kwamba licha ya kilichotokea, bado yuko katika mioyo na akili za watoto wake.

“Ulianzisha uhusiano nao na bado unawatunza katika Nairobi yenye sumu, wewe ni familia. Kwa wale ambao hawajui, tunashiriki asili dhabiti ya familia na kwamba hakuna kinachoweza kutuvunja, "aliandika.

Akothee alibainisha kuwa kama si maandamano ya Sabasaba jijini Nairobi siku ya Ijumaa, angeungana na meneja huyo wake kusherehekea siku yake maalum huku akidokeza kwamba tayari alikuwa ameomba ruhusa ya kufanya hivyo kutoka kwa mumewe Denis Shweizer almaarufu Mister Omosh.

“Yeyote anayekugusa lazima aniue kwanza. Ninaweza kuandika kitabu kizima cha shukrani, kwa ajili yako tu kujua kwamba unathaminiwa, unatambuliwa, unaheshimiwa na unapendwa, tembea na kichwa chako juu, kwa sababu wewe ni fahari ya Kamagambo,” aliandika.

"Kwa kweli, ningekuidhinisha kwa Rongo Mp 2027 ikiwa ningejua mambo ya siasa. Lakini si kikombe changu cha chai, fanya biashara zako na ufurahie maisha yako, ishi maisha ambayo yatakupa furaha na amani."

Kufuatia ujumbe wake kwa mpenziwe huyo wa zamani, mama huyo wa watoto watano alibainisha, "Akili ndogo watafikiri kile wanachotaka kufikiria, lakini ndivyo ilivyo."

View Comments