Ilikuwa ni kicheko asubuhi ya leo, wakati Gidi aliposimulia jinsi mwakilishi wa wadi ya Alego Leonard Oriaro alitoa madai kuwa gavana wa Machakos Alfred Mutua ni wa jamii ya waluo.

Kulingana na bwana Oriaro, jina kamili la babake Alfred Mutua ni Habil Otieno Lut, kutoka kijiji cha Kalenjuok ambacho kiko katika wadi yake. Iisitoshe, Oriaro aliongeza kuwa mjombake Mutua ni mzee wa kijiji chake.

Oriaro pia alidai kuwa jina kamili la Mutua ni Alfred Otieno Odango wala sio Alfred Mutua.

Madai haya ya Oriaro yaliwashangaza watangazaji Gidi na Ghost ambao walichambua madai haya kwa kina.

Skiza kanda hii:

&feature=youtu.be